Writen by
sadataley
8:04 AM
-
0
Comments
Rais Donald Trump ameonywa na wanachama wa chama chake cha Republican kuacha kuingilia uchunguzi maalumu kuhusiana na Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani uliopita.
Hatua hii ya wanachama wa Republican inakuja baada ya rais Trump kumshambulia kuhusiana na uchunguzi wake dhidi ya Urusi kudaiwa kuingilia uchaguzi wa mwaka 2016.
Ktika ukurasa wake wa Tweeter mwishoni mwa juma,Trump alirejea kutoa utetezi wake amesisitiza kuwa hakukuwa na uhusiano wowote kati ya timu yake ya kampeni na Urusi na kusema kuwa hiyo ni vita binafsi inayoshabikiwa na Democrats
Mueller,ambaye ni mkuu wa zamani wa FBI,anaungwa mkono na Republican kuendelea na uchunguzi wake bila kuingiliwa.
iSenata Lindsey Graham amesema Trump asijaribu kufchukua hatua yoyote dhidi ya Muellr.
No comments
Post a Comment