Shirikisho la soka nchni TFF limetangaza kiingilio cha shilingi 1,000, kwenye mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu fainali za AFCON kwa vijana chini ya miaka 20 zitakazofanyika mwaka 2019 nchini Niger.
Mchezo huo ambao utawakutanisha Ngorongoro Heroes dhidi ya Vijanawa DRC Congo utapigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kesho jumamosi ikiwa ni siku nne tu tangu timu ya wakubwa Taifa Stars iifunge nchini hiyo mabao 2-0.
Kikosi cha DRC kimewasili nchini tangu jumatano usiku na kimeendelea kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.
Ngorongoro Heroes iliyo chini ya kocha Ammy Conrad Ninje itaingia kwenye mchezo wa Jumamosi wa kesho kushinda mechi mbili za kujipima dhidi ya Morocco 1-0 na Msumbiji 2-1.
No comments
Post a Comment