UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

Thursday, March 15, 2018

Serikali ya Rwanda imepiga marufuku utoaji adhana

Serikali ya Rwanda imepiga marufuku utoaji adhana, wito kwa waumini wa kiislamu  kudiriki ibada ambao hutolewa mara tano kwa siku kwa madai kuwa wito huo huwa unawakera raia mjini  Kigali.

Uamuzi huo umechukuliwa katika eneo la Nyarugenge, eneo ambalo kunapatikana miskiti mingi mjini Kigali.

Serikali inadai utoaji wa adhana unasababisha kelele nyingi na hivyo misikiti inatakiwa kutafuta njia nyingine ya kuwaita waumini wake.

Hata hivyo bado haijajulikana ni adhabu ipi misikiti itapatiwa endapo adhana zitaendelea kutolewa kama kawaida.

Mufti mkuu nchini Rwanda ameshangazwa sana na tangazo hilo na kusema kuwa suala hilo ni lazima lijadiliwe kwa kina.

Zaidi ya makanisa 800 yamefungiwa nchini Rwanda ndani ya siku chache zilizopita kwa madai ya kutokidhi vigezo na masharti.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment