Serikali ya Afrika kusini imetangaza rasmi ukame na uhaba wa chakula kama majanga ya taifa hilo.
Kwa mujibu wa taarifa waziri Zweli Mkhize amesema kuwa janga hilo limekumba maeneo matatu kati ya tisa Afrika Kusini.
Cape Town, mji muhimu katika masuala ya utalii ni kati ya maeneo yaliyoathiriwa na ukame.
Miji mingine iliyokumbwa na janga hilo ni Northern Cape, Eastern Cape, na the Western Cape.
Afrika Kusini imekuwa ikipata mvua kidogo au mvua kutonyesha kabisa kwa miezi kadhaa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Mabwawa wengi nchini yamepungua kiwango cha maji .
Waziri Mkhize amesema kuwa ni takriban bilioni 6 zilitengwa katika bajeti ya mwaka 2017-2018 kusaidia kupambana na janga hilo.
No comments
Post a Comment