Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, March 18, 2018

Real na Atletico kuchuana Aprili 8


KIPUTE cha wapinzani wa jadi wa jiji la Madrid kinachozikutanisha Real na Atletico kitapigwa Aprili 8, mwaka huu kama ilivyopangwa awali.

Kulikuwa na wasiwasi kuwa mechi hiyo, huenda ikaahirishwa kutokana na ushiriki wa timu hizo kwenye michuano ya Ulaya.

Real Madrid na Atletico Madrid zimefuzu kwa robo fainali ya mashindano ya Ulaya. Real imo Ligi ya Mabingwa wakati Atletico iko kwenye Europa.

Tarehe ya Aprili 8 itakuwa siku ya Jumapili, lakini wiki inayofuata kutakuwa na mechi za robo fainali za michuano ya Ligi ya Mabingwa na ile ya Europa.

Real Madrid iliwasiliana na Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) kuwataarifu juu ya suala hilo lakini wamehakikishiwa kuwa watapangiwa Jumatano ya wiki inayofuata ili kupata muda wa kutosha wa mapumziko.

Hata hivyo, Kamati ya La Liga bado haijapanga muda wa mechi hiyo kwani siku hiyo pia kutakuwepo mashindano ya marathon ya jiji la Madrid.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment