Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa pongezi kwa Bohari ya dawa Tanzania (MSD), baada ya kufanikisha ununuzi wa dawa kwa pamoja na moja kwa moja bila kutumia 'middle men'.
Pongezi hizo amezitoa leo jijini Dar es salaam wakati akizindua magari 181 ya Bohari ya dawa, ambayo yatakuwa yanasambaza madawa na vifaa tiba nchini na kurahisisha upatikanaji wa dawa na vifaa hivyo katika hospitali zote nchini.
''Nawapongeza sana MSD nyinyi mnatekeleza uzalendo vizuri, nasema kwa dhati mmeanza vizuri, mimi ni mgumu kupongeza kwahiyo kama nawapongeza mjue ukweli mnafanya kazi, nakumbuka Mkurugenzi wa MSD na Waziri wa Afya waliniomba fedha ili wawe wananunua dawa wenyewe bila 'Middle men' na wamefanikisha hilo'', amesema.
Aidha Rais Magufuli ametoa ruhusa kwa MSD kufungua maduka yao ya dawa sehemu mbalimbali nchini, lakini wasiyakabidhi kwa halmashauri bali wayasimamie wenyewe hata kama wataongeza wafanyakazi ni sawa tu.
Kwa upande mwingine Rais Magufuli amewalilia wafanyabiashara nchini kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba ili kuokoa kiasi cha zaidi ya bilioni 500 ambazo zinatumika kununua dawa nje ya nchi kila mwaka.
No comments
Post a Comment