Kemikali hizo huathiri mazoa na kudumisha kilimo katika ardhi za wapalestina.
Ndege za Israel za kilimo zanyunyizia kemikali ambazo bado hazijatubulika katika mashamba ya wapalestina yanayopatikana katika Ukanda wa Gaza.
Mkurugenzi wa ardhi na umwagiliaji maji katika idara ya kilimo Nizar al-Wahidi amefahamisha kuwa ndege za Israel zimeanza kunyunyizia kemikali isiotambulika katika mashamba ya wapalestina Ukanda wa Gaza. Kiongozi huyo amesema kuwa ndege hiyo imeanza zoezi hilo na kuelekea katika eneo la Kaskazini huku kemikeli hiyo ikimwagwa. Kwa mujibu wa kiongozi huyo kemekali hiyo inaathiri kilimo na kuaribu mazoa.
No comments
Post a Comment