Wananchi wa Misri wanapiga kura katika uchaguzi wa rais, huku Rais Abdel-Fattah al-Sissi akiwa na uhakika kamili wa kushinda uchaguzi huo. Mpinzani pekee wa Al-Sissi katika kinyang’anyiro hicho ni Moussa Mostafa ambaye ni mwanasiasa asiyejulikana sana, na ambaye tayari aliunga mkono Al-Sissi kuwania urais kwa muhula wa pili. Waliokuwa washindani wakuu katika kinyang’anyiro hicho walijiondoa au kuzuiliwa kushiriki. Upinzani umewataka Wamisri kuususia uchaguzi huo ukiuita kuwa kichekesho. Huku ushindi wa Al-Sissi ukitarajiwa, idadi ndogo ya wapiga kura huenda ikazusha maswali kuhusu kuaminika kwa uchaguzi huo.
No comments
Post a Comment