Writen by
sadataley
9:26 AM
-
0
Comments
Ambrose Mutinhiri, jenerali mstaafu wa jeshi la Zimbabwe na mfuasi wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Robert Mugabe ameunda chama kipya cha siasa kinachojulikana kama Harakati Mpya ya Kizalendo (NFP) kuchuana na rais Emmerson Mnangagwa katika uchaguzi mkuu ujao.
Rais Emmerson Mnangagwa (kushoto) na Robert Mugabe (kulia)
Mutinhiri, ambaye ni veterani wa vita vya uhuru wa Zimbabwe katika miaka ya 1970 alijitoa kwenye chama tawala cha ZANU-PF na kujiuzulu kiti chake cha ubunge siku ya Ijumaa iliyopita na kukutana na Mugabe siku ya Jumapili kumtaarifu juu ya kinachoendelea.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotoa hapo jana, NFP imetangaza kuwa chama hicho kimeundwa na wananchama wa ZANU-PF na Wazimbabwe waliokasirishwa na utaratibu usio wa kikatiba na wa udhalilishaji uliotumika kumuondoa kihalifu uongozini rais Mugabe na wale kiliowataja kama wahalifu halisi walioiharibu bila ya aibu demokrasia inayochipua ya Zimbabwe.
Hayo yanajiri katika hali ambayo duru za karibu na rais wa zamani wa Zimbabwe zimeripoti kuwa Mugabe ana uchungu wa kuondolewa kwenye kiti cha urais alichokalia kwa miaka 37 na kwamba ametangaza uungaji mkono wake kwa chama kipya cha New Patriotic Front (NFP).
Mnamo mwezi Januari mwaka huu rais Emmerson Mnangagwa alitangaza kuwa uchaguzi ujao wa Rais, Bunge na serikali za mitaa nchini Zimbabwe utafanyika katika mazingira huru na ya haki.
Parstoday
No comments
Post a Comment