Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendelo (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe amefunguka na kuweka wazi kuwa Jumapili hii ya matawi imekuwa ni njema kwake na imemuongezea nguvu na ujasiri mpya kuendelea kutetea haki nchini Tanzania.
Mbowe amesema hayo mara baada ya kutoka katika misa ya Jumapili ya matawi ambapo yeye pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya (CHADEMA) Mhe. Edward Lowassa waliweza kusali katika kanisa la Kilutheri Azania Front jijini Dar es Salaam.
"Neno lililotawala leo Jumapili ikiwa ni Jumapili ya Matawi (Mtende) siku 7 kabla ya kufufuka Mesiah, Bwana Yesu Kristo ambayo ni Sikuu Kuu ya Pasaka, lilikuwa ni amani, ili amani ipatikane lazima haki katika familia, haki ndani ya jamii ipatikane, haki uinua taifa, bila haki hakuna amani, hakuna upendo, watawala wajue wakiiminya haki basi wajue hakuna amani,amani ni muhimu sana" alisema Mbowe
Aidha Mbowe aliendelea kusema kuwa "imekuwa Jumapili njema kwangu na iliyonijaza nguvu na ujasiri mpya wa kuendelea kuitetea haki, nawatakia Jumapili njema ya Matawi.
No comments
Post a Comment