Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, March 6, 2018

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un akutana na ujumbe kutoka Korea Kusini

Chung Eui-yong (C), head of the presidential National Security Office, Suh Hoon (2-L), the chief of the South"s National Intelligence Service, and other delegates pose before boarding an aircraft as they leave for Pyongyang at a military airport in Seongnam, south of Seoul, South Korea,

Haki miliki ya pichaEPA
Image captionChung Eui-yong (katikati) na Suh Hoon (wa pili kushoto) ni kati ya wajumbe wanaoelekea Korea Kaskazini
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un anaandaa mkutano wa chakula cha jioni na wajumbe wawili kutoka Korea Kusini, ikiwa ndiyo mara ya kwanza kiongozi huyo anakutana na ujumbe kutoka Kusini tangu aingie madarakani mwaka 2011.
Ujumbe huo uko nchini Korea Kaskazini kwa mazungumzo yasiyo ya kawaida yenye lenngo la kuanzisha mchakato kati ya Korea Kaskazini na Marekani.
Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeboreka kufuata mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi.
Ujumbe huo unawajumuisha maafisa wenye vyeo vya mawaziri - mkuu wa ujasusi Suh Hoon na mshauri wa usalama wa taifa Chung Eui-yong.
Awali Bw Chung aliwaambia waandishi wa habari kuwa atawasilisha azimio la Rais Moon Jae-in la kudumisha mazungumzo na kuboresha uhusiano kati ya Korea Kaskazini na Kusini na kuondoa silaha za nyuklia kutoka Rasi wa Korea.

'Marekani haina haja ya mazungumzo'

Rais wa Marekani Donald Trump alisema Jumapili kuwa Marekani itakuwa tayari kukutana na Korea Kaskazini lakini akasisitiza kuwa Korea ni lazima iondoe zana zake za nyuklia.
Hata hivyo Korea Kaskazini ambayo imesema inataka kufanya mazungumzo na Marekani, imesema kuwa ni hatua ya "kishenzi" kuwa Marekani inataka kuwepo masharti.
Haijulikani ni nani atawakilisha Marekani ikiwa mkutano kama huo utafanyika.
Mjumbe mkuu wa Marekani kuhusu Korea Kaskazini Joseph Yun alitangaza uamuzi wake wa kustaafu mapema wiki iliyopita.
Wadadisi wanaamini kuwa Bw Yun alikuwa akipendelea sana suluhu ya kidiplomasia na Korea Kaskazini.
Joseph Yun (C), US special representative for North Korea policy, answers questions from reporters following a meeting with Japanese and South Korean chief nuclear negotiators at the Iikura Guesthouse in Tokyo on 27 April 2017.Haki miliki ya pichaTORU YAMANAKA/GETTY
Image captionMjumbe mkuu wa Marekani kuhusu Korea Kaskazini Joseph Yun alitangaza uamuzi wake wa kustaafu mapema wiki iliyopita

BBC

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment