Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, March 8, 2018

Jeshi la Polisi Manyara linamshikilia Mbunge Mary Nagu kwa amri ya DC

Leo March 7, 2018 Mbunge wa Jimbo la Hanang, mkoani Manyara Dkt Mary Nagu(CCM) na mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo waanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani humo kwa amri ya Mkuu wa wilaya hiyo kutokana na sababu ya  kushindwa kuelewana kiutendaji.
Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya Sarah Msafiri ameeleza kuwa ameagiza kukamatwa kwa Mbunge huyo baada ya kuchoka kumvumilia kutokana na kauli anazozitoa kwenye mikutano yake na wananchi akihamasisha wasishiriki shughuli za maendeleo.
Pia amemtuhumu Mbunge huyo kuwataka wananchi wasishirikiane naye jambo ambalo alidai ni sawa na kuwataka wananchi wasishirikiane na serikali kwa sababu yeye anasimama kama serikali
“Ni kweli tumemkamata na sababu kubwa ni kuhamasisha wananchi wasishiriki shughuli za maendeleo na pia anawataka wananchi wasishirikiane na Mimi wakati anajua Mimi nasimama kama serikali” -DC Msafiri
Millardayo
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment