Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, March 13, 2018

Aliyejiuzulu Bavicha: Nimejiuzulu nafasi siwezi kuacha siasa


Dar es Salaam. Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Gertrude Ndibalema amesema licha ya kujiuzulu wadhifa huo, hana mpango wa kuachana na siasa.

Akizungumza na MCL Digital leo Jumanne Machi 13, 2018  amesema siasa ni maisha na ni ngumu kwake kama kijana kuachana nayo, “nisiposikika katika ulingo huo wa siasa nitaonekana tu. Siwezi kufanya uamuzi wa ajabu kama huo wa kuacha siasa, nimejiuzulu nafasi hiyo, lakini mimi bado ni mwanasiasa ukizingatia umri unaniruhusu.”

Amesema katika nafasi ya uongozi aliyokuwa nayo changamoto zilikuwa nyingi, lakini alikuwa anatoa ushauri kwa viongozi wa chama na kwamba zipo zilizofanyiwa kazi na ambazo hazijafanyiwa kazi.

Kuhusu demokrasia nchini amesema, “Nchi ili iwe na  demokrasia lazima iwe na siasa safi na uongozi bora, swali la kujiuliza ni kwamba Tanzania kuna vitu hivyo viwili.”

“Kama hakuna vitu hivyo ina maana bado hatuna demokrasia, kuna kukatazwa mikutano ya siasa, kukatazwa maandamano, kuna vitu vichache vikifanyiwa kazi kila kitu kitakuwa sawa.”

Gertrude aliyeshika wadhifa huo tangu mwaka 2014 alitangaza kujiuzulu Machi 12, 2018 kupitia taarifa kwa umma akidai anabaki kuwa mwanachama ili kutimiza majukumu yake binafsi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment