Writen by
sadataley
12:55 PM
-
0
Comments
Mkurugenzi wa Shirika la Watumishi Housing Company Dk. Fredy Msemwa akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya shirika hilo jengo la Golden Tower jijini Dar es salaam wakati akitangazo mradi mpya wa Njedengwa mjini Dodoma ambapo zinajengwa nyumba za awali 154 eneo hilo litajengwa zaidi ya nyumba 500 , kulia ni Aisa Mawasiliano na Mauzo wa Shirika hilo Bi Maryjane Makawia.
Mkurugenzi wa Shirika la Watumishi Housing Company Dk. Fredy Msemwa akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya shirika hilo jengo la Golden Tower jijini Dar es salaam wakati akitangazo mradi mpya wa Njedengwa mjini Dodoma ambapo zinajengwa nyumba za awali 154 eneo hilo litajengwa zaidi ya nyumba 500, Kutoka kulia ni Afisa Mauzo Irene Kasanda na Afisa Mawasiliano na Mauzo wa Shirika hilo Maryjane Makawia.
Bw. Raphael Mwabuponde Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo akiwaelezea waandishi wa habari jinsi mradi huo wa nyumba utakavyotekelezwa.
……………………………………………………………………………
Kampuni ya Watumishi Housing Company, yenye dhamana ya uwekezaji katika nyumba na inayotekeleza mpango wa taifa wa makazi kwa Watumishi, ina jukumu la kujenga nyumba 50,000 zitakazouzwa kwa mikopo nafuu ya muda mrefu kwa watumishi waishio ndani na nje ya nchi. Mpaka sasa WHC imeishajenga nyumba maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni awamu ya kwanza katika kutekeleza mpango wa taifa wa makazi kwa watumishi na maeneo yaliyojengwa mpaka sasa ni Morogoro Mkundi (50), Kisesa Mwanza (59), Magomeni Dar Es salaam (88), Bunju B Mwabepande (64), Gezaulole Kigamboni (329) na sasa kuanza ujenzi wa nyumba (159) katika makao makuu Dodoma .
Katika kuunga mkono uamuzi wa serikali wa kuhamishia shughuli za serikali katika mkoa wa Dodoma kwa nia ya kuboresha maendeleo ya nchi, Watumishi Housing tumejipanga kuwajengea watumishi nyumba bora na za kisasa mkoani Dodoma katika eneo la Njedengwa, lililopo mkabala na eneo la Kisasa Dodoma.
Kutokana na mpango wa serikali wa kuhamishia shughuli zake mkoani Dodoma kuja na fursa nyingi ikiwa moja wapo ni ya kuendeleza makazi ya watumishi ambapo kwa sisi WHC ni jukumu la msingi sana kwetu kuhakikisha watumishi wanapata makazi bora na ya kisasa kwa bei nafuu. Hivyo basi kutokana na fursa hii Watumishi Housing imeandaa ardhi ya ekari 55 za ardhi katika mkoa wa Dodoma ambapo tunategemea kujenga jumla ya nyumba 500. Nyumba 159 zitajengwa katika awamu ya kwanza kwaajili ya watumishi watakao kuwa wakihamia Dodoma na wale wanaoishi Dodoma. Bei ya nyumba ya vyumba vitatu itaanzia shs millioni 46.
Njedengwa ni eneo ambalo limeendelezwa tayari likiwa na barabara za lami, maji, umeme na miundo mbinu mingine ambayo inalifanya kuwa eneo bora zaidi kwa makazi ya watumishi. Ujenzi wa nyumba za watumishi umeishaanza katika mkoa wa Dodoma na wiki hii tumemaliza ‘site clearance’, ujenzi wa nyumba hizi utachukua muda wa miezi 8 kukamilika. Nyumba tunazotegemea kujenga zitakua za aina mbili. Zilizoisha kabisa (full finished) na zile zitakazokua zimeisha kwa asilimia 80% ambapo mtumishi atakua na fursa ya kuingia na kuishi huku akimalizia kwa kadri anavyopenda. Na tumeamua kufanya hivi ili kuweza kuwasaidia Watumishi wenye vipato vya chini na wangependa kumiliki nyumba kwani nyumba hizi zitakua na bei nafuu zaidi. Nyumba zote zitakua za vyumba vitatu vya kulala, ambapo kwenye nyumba utapata chumba kimoja cha kujitegemea au masterbedroom, vyumba vingine vya kawaida, sebule, sehemu ya kula chakula au dining room, choo, bafu, jiko, store, veranda upande wa nyuma na mbele ya nyumba, eneo la maegesho ya magari pamoja na garden.
Bei za nyumba zilizokamilika kabisa itakua shs milioni 58 pamoja na VAT na zile ambazo zimekamilika kwa asilimia 80% tayari kwa kutumika zitauzwa shs milioni 46 pamoja na VAT na zitauzwa kwa njia ya malipo enedelevu wakati wa ujenzi au kwa mkopo wa bei nafuu toka benki washirika na kurejeshwa ndani ya mwaka mmoja hadi miaka 25. Watumishi watakaopenda kumiliki nyumba hizi tunawaomba wachukue fomu za maombi katika ofisi zetu zilizopo jengo la Golden Jubilee ghorofa ya 4 au katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Dodoma au watembelee tovuti yetu www.whctz.org, Vilevile fomu za maombi zinapatikana katika wizara na ofisi za halmashauri zote nchini.
Vilevile Watumishi Housing tumepata msaada wa vifaa vya upimaji wa viwanja na miji hivyo basi WHC itatoa huduma zote za makazi kuanzia uuzaji wa viwanja vilivyopimwa pamoja na nyumba zilizokamilika. Kwa kuanzia huduma ya uuzaji wa viwanja itaanza kwa kuwahudumia Watumishi wa umma mkoani Dodoma na huduma hii itaambatana na huduma zingine za ushauri wa ramani za nyumba.
Watumishi Housing tunashauri watumishi kununua nyumba tayari zilizojengwa na zilizo bora na za kisasa badala ya kununua ardhi na kuanza ujenzi. Kwakufanya hivi utakua unanunua nyumba ambayo tayari imeishajengwa kwa ubora na kisasa kwa bei nafuu kabisa vilevile utakua unaondokana na matatizo mengi sana yanayokuja na ujenzi kama kupoteza muda, gharama kubwa na n.k.
No comments
Post a Comment