Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba ameagiza kutaifishwa kwa magari na boti ambazo zitabainika kusafirisha hamiaji haramu wanaoingia nchini kinyume na sheria na kwa wale ambao watakuja kuwalipia faini nao wachukuliwe hatua za kisheria.
Waziri Nchemba ametoa kauli hiyo akiwa mkoa wa Pwani katika ziara ya kikazi ambapo alikagua Kiwanda cha kuchapisha Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Pwani.
Mh. Nchemba ameagiza kuanzia leo mtu atayejitokeza kuwalipia faini wahamiaji haramu ili waachiwe naye ajumuishwe nao, na vifaa ambavyo vimetumika kuwa safirisha wahamiaji haramu vitaifishwe na kupewa idara ya magereza na katika idara nyingine zenye maitaji ya vifaa.
Akiwa katika kiwanda cha NIDA, Waziri Mwigulu amesema kiwanda hicho kimekamilika kwa asilimia 99.9 na ni jengo kubwa lenye hadhi ya kitaifa ambalo litatumika kufanikisha upatikanaji wa vitambulisho kwa kila mwananchi.
Aidha Mwigulu Nchemba amedai Kwa sasa wananchi hutumia vitambulisho vingi lakini sasa kutakuwa na kitambulisho kimoja na taarifa zake tangu anazaliwa mpaka anakuwa anamiliki kiwanda au anafanya shughuli nyingine taarifa zake zote zinakuwa zimehifadhiwa zinajulikana.
No comments
Post a Comment