Writen by
sadataley
12:52 PM
-
0
Comments
Kocha Mkuu wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa kikosi chake kinaweza kushinda ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza baada ya msimu uliopita kufanya vibaya na kumaliza kwenye nafasi ya nne ambayo imewapa nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Liverpool ilianza msimu wa 2016-17 vizuri na walikuwa pointi sita pekee nyuma ya viongozi na hatimaye bingwa wa ligi Chelsea mnamo mwezi Januari.
Lakini walirudi nyuma baada ya kupata ushindi mmoja mwezi Januari na Februari kabla ya kumaliza katika nafasi ya nne pointi 17 nyuma ya Chelsea.
”Tutashiriki mechi za ubingwa.hatutaki kuanza msimu bila kuwa na lengo lolote”, alisema Klopp.
“Lazima tuwe na lengo na nadhani tuna timu nzuri sana sasa.tulikuwa na bahati mbaya msimu uliopita”.
”Nadhani tunaweza kucheza vyema .Tuwe na matumaini kwamba kila kitu kitakuwa shwari. Klop alisema kuwa kwamba mchezaji Phillipe Coutinho hauzwi, licha ya Barcelona kumtaka”.
No comments
Post a Comment