Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr. Hamisi Kigwangalla amesema mkojo waweza kuwa na uhusiano na vitendo vya uchochezi.
Akifafanua suala hilo baada ya mdau kuuliza kwa njia ya mtandao. Je kipimo cha mkojo kinaweza kugundua vimelea vya uchochezi?
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Dr. Kigwangalla alijibu kuwa
"Huwezi kujua, pengine mtu akiwa kwenye 'influence' ya dawa ndiyo anakuwa na propensity ya 'uchochezi' ikigundulika ndivyo anaweza kusaidiwa.
"Ukiwa hujui sayansi unaweza kudhani mkojo hauna uhusiano na vitendo vya uchochezi! Raia mwema huwezi kukataa kipimo chochote, labda mharifu",
Uchochezi waweza kuwa na uhusiano na matumizi ya kemikali zenye kuvuruga akili, hili liko wazi labda uwe mbumbumbu wa sayansi au nyumbu!
aliandika Dr. Kigwangalla.
No comments
Post a Comment