Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, July 23, 2017

Askofu Gaville: Katiba mpya ndiomuarobaini wa ufisadi

Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Blaston Gaville (kushoto).

KUKAMILIKA kwa mchakato wa uaandaaji wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutasaidia kuweka misingi imara na kuondoa changamoto zilizopo katika Katiba ya sasa, hivyo kukomesha ufisadi na kuinua uchumi wa Tanzania.

Aidha, kukamilika huko kwa Katiba Mpya kutaakisi jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.

Hayo yalisemwa hivi karibuni na Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Blaston Gaville, ambaye alimtaka Rais Magufuli kuumalizia mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya, kwani alisema mbali ya kuakisi kasi yake anayoifanya ya kukuza uchumi pia kutasaidia kuhimiza uwajibikaji.

“Wakristo na Watanzania kwa ujumla tuna imani kubwa na Serikali ya Awamu ya Tano na ni matarajio yetu kwamba mchakato wa kuandika Katiba utamalizwa kama lengo lilivyokuwa,” alisema.

Askofu Gaville amesimikwa ili kuchukua nafasi ya Askofu Dkt. Owdenburg Mdegella ambaye amestaafu.Alisema wanatiwa moyo na jitihada zinazoendelea kufanywa na Dkt. Magufuli katika kufufua uchumi na kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kwa manufaa ya Watanzania wote.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment