Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, June 29, 2017

Selemani Matola aula Lipuli Fc

KOCHA mpya wa Lipuli FC ya mkoani Iringa, Selemani Matola, ameeleza kuwa, tayari ameshaanguka wino wa kuitumikia Lipuli kwa mkataba wa mwaka mmoja na kudai kuwa, anahitaji kukifanyia mabadiliko kikosi hicho kwa kuhakikisha anasajili wachezaji vijana.

Lipuli ni miongoni mwa timu tatu zilizopanda daraja msimu uliopita, ikiwa ni pamoja na Njombe Mji ya Iringa na Singida United baada ya kufanya vyema Ligi Daraja la Kwanza.

Matola alisema kuwa, baada ya kufanikiwa kusaini mkataba katika klabu hiyo, moja ya kazi atakazoanza nazo ni kuhakikisha anakifanyia uboreshaji kikosi hicho kwa kusajili wachezaji vijana huku akibakiza wachache walioipandisha timu daraja.

Natarajia kwenda Iringa wakati wowote, kwa sasa kuna programu ambayo nahitaji kuifanya kwa ajili ya suala zima la usajili, ya kwanza nitaanza nayo hapa na nyingine nitaenda kuifanyia Iringa lakini nitaangalia ndani ya siku mbili hizi ndiyo nitaweza kutoa majibu rasmi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment