Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, April 15, 2017

Tiba Bora Ya Mwili Na Afya Yako Ni Hii Hapa

Kuna wakati kama binadamu huwa tunapatwa na magonjwa ya aina mbalimbali. Yapo magonjwa ambayo huwa tunajua chanzo na tiba yake na mengine huwa hatujui. Kwa kuwa afya ni muhimu sana kwa binadamu, kila mtu hufanya kila linalowezekana kuhakikisha mwili wake uko salama kiafya.

Katika kuhakikisha hili linatimia wapo ambao hutumia dawa za kila aina na wapo pia wengine ambao huamua kutumia tiba mbadala. Yote haya hufanyika ili kupata tiba bora ya mwili na afya zetu. Katika makala hii ya leo tutaangalia tiba nyingine bora ya mwili ambayo haifahamiki na wengi. Tunasema ni bora kwa sababu inatibu magonjwa mengi. Tiba hii ni tiba ya zabibu.

Ikumbukwe Zabibu hulimwa sehemu nyingi sana duniani. Matunda ya zabibu ni matamu sana kwa maana ya ladha nzuri mdomoni. Zabibu ziko za kijani, nyeusi na urujuani(Violet). Pia ziko katika maumbile na ‘saizi’ mbalimbali. Kuna zile zenye maumbile madogo na zina mbegu ndogo na nyingi.

Zabibu ni nzuri sana kwa matatizo ya koo, nywele, ngozi na matatizo ya macho. Vilevile zabibu inaleta hamu ya kula. Zabibu zinasaidia kuondoa kiu, homa, pumu, ukoma, kifua kikuu, matatizo ya sauti na kutapika. Inapunguza gesi tumboni.

Zabibu zinaharibika upesi baada ya kuiva hivyo zinataka matunzo mazuri kwa kuwekwa jokofu au penye baridi baada ya kuvuna. Ili zabibi ifanye kazi, huna budi kuzila nyingi kwa siku. Zabibu hufanya mtu aonekane kijana kwa muda mwingi. Glucose iliyo kwenye zabibu huyeyuka kwa haraka sana mwilini.

Zabibu zinasaidia kwenye mambo mengi sana kama unywaji pombe kupita kiasi yaani ‘Alcoholism’. Matatizo ya unywaji pombe mara kwa mara au kupita kiasi unaweza kuachwa au kupunguzwa kwa kula zabibu kila siku. Zabibu zenyewe zinatoa pombe mwilini.

Harufu ya zabibu inaleta ahueni kwenye kwenye matatizo ya pumu na matatizo ya watoto wadogo. Juisi ya zabibu inasaidia kutibu matatizo ya choo kwa watoto wadogo, hata kwa wakubwa inasaidia. Zabibu inasaidia kupunguza matatizo ya moyo na matatizo ya figo.

Zabibu pia inasaidia matatizo ya ini kwa sababu ina tindikali aina ya Malic, Citric na Tartaric. Tindikali hizi zinasaidia kusafisha damu, kuamsha ufanyaji kazi wa tumbo na ini.

Hayo ndiyo magonjwa yanayoweza kutibiwa kwa kutumia Zabibu. Hivyo, ni muhimu sana kwa miili yetu.

Tunakutakia siku njema na afya bora, ila kama umesoma makala hii mshirikishe na mwingine ili apate tiba hii bora bila kuikosa.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment