Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, April 13, 2017

MATUKIO YA KUMBUKUMBU YA HAYATI SOKOINE ILIYOFANYIKA WILAYANI MONDULI

pam1
Msaidizi wa Askofu, jimbo kuu Katoliki Arusha, Prosper Lyimo akiweka shada la maua kwenye kaburi la Waziri Mkuu wa zamani, Hayati Edward Moringe Sokoine wakati wa ibada ya kumbukumbu ya kifo cha kiongozi huyo miaka 33 iliyopita, iliyofanyika nyumbani kwa Sokoine wilayani Monduli.
pam2
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye ibada ya kuadhimisha miaka 33 ya kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania, Hayati Edward Sokoine, wilayani Monduli.
pam3
Mke wa kwanza wa Sokoine Mama Napono katrika, na wa pili Mama Nekiteto kulia, wakizungumza na waziri wa maliasili na utalii Jumanne Maghembe nyumbani Wilayani Monduli
pam4
Msaidizi wa Askofu, Prosper Lyimo akihubiri wakati wa ibada ya kuadhimisha miaka 33 ya kifo cha Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Sokoine
pam5
Binti wa Sokoine, Namelok na Kaka yake, Balozi Joseph Sokoine wakiwa na wageni wengine walioshiriki ibada ya kumbukumbu ya baba yao wilayani Monduli.
pam6
Wake za marehemu wakiwa wanaweka taji katika kaburi la Hayati Edward Sokoine, wilayani Monduli.
pam7
Wake za marehemu wakiwa wanaweka taji katika kaburi la Hayati Edward Sokoine, wilayani Monduli.
pam8
Mwakilishi wa mkuu wa Majeshi Tanzania, Brigadia Jenerali, Anderson Ghulila akiwa anawekataji katika kaburi la Hayati Edward Sokoine, wilayani Monduli katika ibada ya kumbukumbu ya kifo cha kiongozi huyo miaka 33 iliyopita, iliyofanyika nyumbani kwa Sokoine
pam9
Wajukuu wa Hayati Edward Sokoine wakiwa katika ibada ya kumbukumbu ya kifo cha kiongozi huyo miaka 33 iliyopita, iliyofanyika nyumbani kwa Sokoine
pam10
Mtoto wa Hayati Sokoine, Balozi Joseph Sokoine akizungumza na wageni waalikwa katika misa maalum ya kumuenzi baba yake.
pam11
Baadhi ya wageni kutoka sehemu mbalimbali waliohudhuria misa ya kumbukumbuku ya Sokoine.
pam12
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka akibadilishana mawazo na mwakilishi wa mkuu wa Majeshi Tanzania, Brigadia Jenerali, Anderson Ghulila pamoja aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, Balozi Daniel Ole Njoolay
pam13
Baadhi ya viongozi walioshiriki ibada ya kumbukumbu ya miaka 33 ya Sokoine, kutoka kushoto ni Askofu wa Dayosisi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Mkoani Arusha, Solomon Masagwa, Mwakilishi wa Shehe Mkuu, Rajab Kiungiza, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka na Waziri wa Maliasili na Utalii Jumanne Maghembe kwenye picha ya pamoja
pam14
Wanakwaya wakiandamana kuelekea eneo la ibada tayari kwa Misa Maalum.(PICHA ZOTE NA PAMELA MOLLEL ARUSHA)
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment