Writen by
sadataley
1:15 PM
-
0
Comments
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi, Naibu wake Mhe. Dkt. Angeline
Mabulla, Katibu Mkuu; Dkt Yamungu Kayandabila na Viongozi wengine wakuu
wa wizara wakikagua magari ya kuhudumia ofisi za ardhi za kanda nchini.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akikabidhi funguo ya gari kwa
Kamishna wa kanda ya Dar es Salaam; Matthew Nhone.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi, Naibu wake Mhe. Dkt. Angeline
Mabulla, Katibu Mkuu; Dkt Yamungu Kayandabila na Viongozi wengine wakuu
wa wizara wakikagua magari ya kuhudumia ofisi za ardhi za kanda nchini.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi imeboresha ofisi zake za kanda za ardhi zilizopo
nchini ili kuongeza ufanisi katika kutoa huduma za ardhi karibu zaidi na
wananchi.
Wizara imegawa magari katika kanda
zake zote ili kurahisisha utekelezaji wa kazi za ardhi na kuharakisha
huduma za sekta nzima ya ardhi katika maeneo yote ya nchi badala ya
wananchi kuja ofisi za Dar es Salaam ambazo kwa sasa zinahamia makao
Makuu ya Nchi Dodoma. Hatahivyo, huduma nyingine za kisekta kama vile za
malipo ya kodi ya pango la ardhi, kituo cha huduma kwa mteja na ofisi
za kanda za Dar es Salaam zitaendelea kufanyika kama ilivyokuwa awali.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati akitangaza kuhamia rasmi
kwa Wizara yake mkoani Dodoma amesema kuwa Wizara imepanga kuwaweka
wataalam wa sekta nzima ya ardhi katika ofisi za kanda ili kuondoa
usumbufu uliokuwepo wa kufuata huduma za hati, usajili, Uthamini upimaji
na ramani na mipango miji na vijiji – Dar es Salaam na Dodoma.
Katika kutekeleza hili kila Kanda
itakuwa na viongozi wake walio na mamlaka za utoaji wa huduma za ardhi
na kuidhinishwa kwa nyaraka mbalimbali za ardhi na hata utoaji wa hati
miliki kutolewa katika kanda.
Viongozi ambao watakuwepo katika
kanda hizo ni pamoja na Kamishna na Kanda Msaidizi wa Ardhi, Msajili
Msaidizi wa Hati wa Kanda, Mthamini Mkuu Msaidizi wa Kanda, Mkurugenzi
Msaidizi wa Upimaji na Ramani wa Kanda, Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango
Miji na Vijiji wa Kanda na Msajili Msaidizi wa Baraza la Ardhi na Nyumba
wa Kanda.
Aidha jumla ya kanda ni nane
ambazo ambazo zimeboreshwa na kuundwa upya. Kanda hizo ni; Kanda ya Dar
es Salaam na Pwani, ambayo itahusika na mikoa ya Dar es Salaam na Pwani,
na Dar es Salaam ndio makao makuu ya kanda. Kanda ya Nyanda za Juu
Kusini; itahusika na mikoa ya Mbeya, Njombe, Rukwa na Songwe, ambapo
Mbeya ndio makao makuu ya kanda. Kanda ya Kati; ni pamoja na mikoa ya
Dodoma, Singida, Iringa na Morogoro na Dodoma ni makao yake makuu.
Aidha, Kanda ya Kaskazini; ni
mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Manyara, ambapo makao yake makuu
ni Arusha. Kanda ya Ziwa; Ni mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera, ambapo
Mwanza ndio makao yake makuu. Nyingine ni Kanda ya Magharibi; yenye
mikoa ya Tabora, Kigoma na Katavi na Tabora ndio makao makuu ya kanda.
Kanda ya Kusini; Ni mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma na Mtwara ndio
makao makuu ya kanda, na kanda ya nane ni Simiyu; yenye mikoa ya Simiyu,
Shinyanga na Mara na Simiyu ndio makao makuu.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
No comments
Post a Comment