Writen by
sadataley
1:13 PM
-
0
Comments
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Maafisa wa Idara ya
Uhamiaji Zanzibar, wakati wa ziara ya kukagua udhibiti wa uingiaji wa
Dawa za Kulevya Visiwani humo, huku akiagiza vyombo vya ulinzi na
usalama kushirikiana kudhibiti madawa hayo ambayo yanaharibu nguvu kazi
ya Taifa.
Kamishna wa Jeshi la Polisi
Zanzibar, Hamdan Omar Makame, akitoa taarifa za utekelezaji wa zoezi la
kudhibiti Dawa za Kulevya Visiwani humo kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), wakati wa ziara ya
naibu waziri kufuatilia utekelezaji wa zoezi la kudhibiti uingiaji wa
dawa za kulevya Visiwani humo.
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji
anayesimamia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume,
Fulgenze Mutarasha, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni (wakwanza kushoto), juu ya hatua
zinazochukuliwa na Idara ya Uhamiaji na vyombo vingine vya Ulinzi na
Usalama kukabiliana na udhibiti wa uingiaji wa Dawa za Kulevya kiwanjani
hapo.Wapili kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mohamed Ahmada Salum na
anayefuatia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akisikiliza jinsi
mifumo ya kudhibiti uingiaji haramu inavyofanya kazi kutoka kwa Mkuu wa
Idara ya Uhamiaji anayesimamia Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume,
Fulgenze Mutarasha.Ziara ya Naibu Waziri huyo ilikua na lengo la kukagua
mifumo inayotumika kudhibiti uingiaji wa Dawa za Kulevya
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akitoa maelezo kwa watumishi wa
Idara ya uhamiaji waliopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani
Karume wakati wa ziara ya ukaguzi wa mifumo ya kudhibiti uingiaji wa
Dawa za Kulevya Visiwani Zanzibar.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akiteta jambo na Naibu Waziri
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar,Mohamed Ahmada Salum wakati wa ziara ya ukaguzi wa mifumo ya
kudhibiti uingiaji wa Dawa za Kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Sheikh
Abeid Amani Karume.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments
Post a Comment