Writen by
sadataley
1:17 PM
-
0
Comments
Mtaalam kutoka Sehemu ya Nishati
Jadidifu, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Stephan Kashushura
(kulia) akibadilishana mawazo na Sister Richardis Chiwinga katika ziara
ya wataalam wa nishati jadidifu katika mradi wa kuzalisha umeme kwa
kutumia maji wa Benedict Sisters of Saint Agnes Chipole, Mbinga mkoani
Ruvuma.
Sister Richardis Chiwinga kutoka
katika mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Benedict Sisters of
Saint Agnes Chipole (katikati) akielezea hali ya maji katika bwawa la
mradi huo kwa wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na
Madini.
Sehemu ya bwala la maji katika
mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Benedict Sisters of Saint
Agnes Chipole, Mbinga mkoani Ruvuma.
Sister Richardis Chiwinga kutoka
katika mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Benedict Sisters of
Saint Agnes Chipole (kushoto) akiongoza watalam kutoka Idara ya Nishati
Jadidifu, Wizara ya Nishati Jadidifu katika ziara kwenye eneo la mradi.
Moja ya mitambo ya kuzalisha
umeme kwa kutumia maji katika mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji
wa Benedict Sisters of Saint Agnes Chipole.
Meneja Uendeshaji kutoka kampuni
ya kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko madogo ya maji ya kampuni ya
Rift Valley Energy, Joel Gomba (kulia) akionesha sehemu ya kuchepushia
maji katika mradi wa Luponde Hydro Ltd uliopo katika hatua ya ujenzi
mkoani Njombe kwa mtaalam kutoka Sehemu ya Nishati Jadidifu, Wizara ya
Nishati na Madini, Emillian Nyanda (kushoto).
………………………………………………………………….
Na Greyson Mwase, Njombe
Kaya 1600 katika vijiji kumi
mkoani Njombe zinatarajiwa kupata umeme wa uhakika mara baada ya
kukamilika kwa mradi wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia maporomoko ya
maji wa Luponde Hydro Ltd unaotekelelezwa na kampuni ya Rift Valley
Energy.
Hayo yalielezwa leo na Meneja
Mradi wa Luponde Hydro, Mugombe Maxwell katika ziara ya wataalam wa
nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini katika mkoa wa
Njombe ili kujionea maendeleo ya miradi midogo ya umeme wa maporomoko
ya maji na nishati jadidifu inayotekelezwa katika mkoa huo.
Maxwell alisema kuwa kampuni ya
Rift Valley Energy ina miradi miwili ambayo ni Mwenga Hydro Grid wenye
uwezo wa Megawati 4.1na Luponde Hydro Ltd utakaokuwa na uwezo wa
kuzalisha Megawati 3 mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wake hivyo
kuwezesha vijiji kumi katika mkoa huo kupata umeme wa uhakika ifikapo
mwakani.
Akielezea mradi huo wa Luponde
Hydro Ltd, Maxwell alisema kuwa mradi ulianza mwaka 2016 na kuongeza
kuwa mradi huo upo katika maeneo mawili ambayo ni Luhololo na Igola yote
yakiwa mkoani Njombe.
Akielezea ujenzi wa mradi huo,
Maxwell alieleza kuwa mradi umegawanyika katika awamu mbili na
kuendelea kusema kuwa awamu ya kwanza inahusisha usambazaji wa umeme wa
uhakika katika vijiji saba vyenye kaya 1120, shule tisa na vituo vya
afya vitano
Aliongeza kuwa, awamu ya pili inahusisha usambazaji wa umeme wa uhakika katika vijiji vitatu vyenye kaya 180.
Akielezea hatua iliyofikiwa ya
utekelezaji wa mradi huo, Maxwell alisema kazi katika eneo la Luhololo
imekamilika kwa asilimia 60 kwa kazi za kawaida na asilimia 40 katika
ujenzi wa mitambo.
Aliongeza kuwa katika eneo la
Igola mradi umekamilika kwa asilimia 40 na kusisitiza kuwa kampuni
itahakikisha kuwa ujenzi katika maeneo yote unakamilika ifikapo mwakani
ili wananchi wapate umeme wa uhakika.
Alisisitiza kuwa lengo la mradi
ni kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na umeme wa uhakika na kuchangia
ukuaji wa uwekezaji kwenye viwanda hususan katika maeneo ya vijijini,
hivyo kuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.
No comments
Post a Comment