Writen by
sadataley
1:12 PM
-
0
Comments
Kikao cha kawaida cha Kamati ya
Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kinatarajiwa
kukaa Machi 26, mwaka huu ambako pamoja na ajenda nyingine, itaamua
tarehe rasmi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu.
Kikao hiki cha kawaida, kwa
mujibu wa katiba hufanyika mara nne kwa mwaka na huamua masuala
mbalimbali ya uendeshaji na usimamizi wa mpira wa miguu nchini.
Kadhalika Mkutano Mkuu wa uchaguzi kwa mujibu wa Katiba ya TFF, hufanyika kila baada ya miaka minne kwa mwaka.
Chanzo:Fullshangwe Blog
No comments
Post a Comment