Writen by
sadataley
1:04 PM
-
0
Comments
Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph
Chitinka akiwasalimia wachezaji wa timu ya Waandishi wa habari mkoa wa
Iringa (IMFC) kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya kijiji cha
Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya
Mbuzi
Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph
Chitinka akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Waandishi
wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu
ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye
mashindano ya Mbuzi Cup
Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph
Chitinka akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya kijiji
cha Mangalali kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya Waandishi wa
habari mkoa wa Iringa (IMFC) uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye
mashindano ya Mbuzi Cup.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MASHINDANO ya kombe Mbuzi Cup
yatafikia tamati tarehe 30 mwezi wa tatu kwa kuzikutanisha timu za
Mkwawa Rangers na Waandishi wa habari mkoa wa Iringa na fainal hiyo
itachezwa katika kijiji cha Kalenga kata ya Kalenga wilayani Iringa
mkoani Iringa ikiwa lengo la kuinua vipaji wa wachezaji kata hiyo.
Akishudia mchezo wa nusu fainal
kati ya timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) na timu ya
kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga katibu
tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka ambaye alikuwa mgeni rasmi
alisema ni wakati mzuri kwa sasa kuyageukia mashindano ya mchangani
kwani yamesheheni vipaji vingi vitakavyosaidia kuendeleza mpira wa
Tanzania wakati ambapo taifa likiendelea kupata matokeo yasiyoridhishwa
kwenye soka kwa sasa,
“Mashindano haya ni muhimu sana
kwa wakati huu kwani yatasaidia kuinua vipaji vya vijana wetu na kuweza
kupata timu bora ya taifa hivyo nidhamu ni muhimu wakati wa michezo
hiyo” alisema Chitinka
Aidha Chitinka aliongeza kwa
kusema kuwa mpira wa miguu umekuwa na faida kwa wachezaji kwani wanaweza
kujitengezea vyanzo vya ajira kama mbwana samatta na wachezaji wengine
walipwa vizuri saizi hapa nchini hata nje ya nchi.
“Mwaka huu tumekuja na wataalamu
wanachagua vipaji maalumu kwaajili ya kujiunga na timu mbalimbali na
lengo likiwa ni kuhakikisha vipaji vyote vinaonekana na vinafika mbali
kwa kuwa sasa mpira ni ajira si mnamuana mchezaji Mbwana
Samatta”.alisema Chitinka
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano
hayo Obeid Msigwa aliwataka washiriki wa mashindano hayo kujituma ili
ipatikane timu ya bora ambayo itakuwa ikiwakilisha katika mashindano ya
mbalimbali.
“Soka imewapa ajira mamilioni ya
wachezaji na viongozi ulimwenguni na wameweza kuishi maisha ya kifahari
kutokana na mishahara wanayopata”, alisema Msigwa
Kwa upande wake mlezi wa
mashindano hayo kamanda wa vijana wa chama cha mapinduzi (ccm) wilaya
Iringa Jackson Kiswaga alisema ataendelea kwaunganisha vijana kupitia
michezo na kusaidia kukuza mpira wa wilaya ya Iringa.
“Ilani ya chama cha mapinduzi
inatutaka mwenyeviti kote nchini kuhakikisha michezo inafanyika mara kwa
mara na kuleta tija kwa taifa ili tuondokane kuwa kuwa vichwa vya
wendawazimu”alisema Kiswaga.
Mashindano ya Mbuzi Cup ni
miongoni mwa mashindano yanayolenga kuibua vipaji vya vijana vijijini
ili kuwawezesha kupata nafasi ya kucheza katika vilabu vikubwa nchini.
No comments
Post a Comment