Writen by
sadataley
1:16 PM
-
0
Comments
Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi,Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wananchi wa Jimbo la Rifiji Mkoani Pwani.
Mbunge wa Jimbo la Rufiji,Mohamed Mchengerwa (CCM) akizungumza na wananchi wa eneo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Rufiji,Mohamed Mchengerwa (CCM) akizungumza na wananchi wa eneo hilo.
Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi,Profesa Joyce Ndalichako akiwa na Mbunge wa Jimbo la Rufiji,Mohamed Mchengerwa (CCM) wakiongozama na wanafunzi wa sekondari ya Utete.
Waziri
wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi,Profesa Joyce Ndalichako,amesema
serikali inatarajia kuajiri walimu wa masomo ya sayansi zaidi ya 4000
ili kupunguza tatizo la uhaba wa walimu hao nchini.
Profesa
Ndalichako aliyasema hayo juzi katika ziara yake Wilayani Rufiji ambapo
ambapo alieleza kuwa kipaumbele kitatolewa katika shule za wilaya hizo
ambazo kila aliyotembelea alikuta zina uhaba wa walimu hao na zingine
hazina kabisa kwa miaka zaidi ya mitano.
Akiwa
katika Shule ya Sekondari Utete ambapo aliongozana na Mbunge wa Jimbo
la Rufiji,Mohamed Mchengerwa (CCM) alieleza kusikitishwa na kufeli kwa
wanafunzi wengi katika mitihani ya kidato cha nne Mwaka jana na
kuwaeleza kuwa serikali itajitahidi kutatua changamoto zilizopo ili
wanafunzi wasipate kisingizio cha kufeli.
‘’Jitihada
za Mbunge wenu anavyowaongelea ndani ya bunge zimenileta hapa leo
kutokana na serikali hii kuwa sikiivu lakini nimesikitishwa na matokeo
yenu ya Mwaka jana mmefeli sana lakini nimeona changamoto zilizopo
katika shule yenu ikiwemo ukosefu wa walimu hasa wa sayansi,kutokuwepo
kwa vifaa vya maabara tutawaletea mwezi huu na uchakavu wa vyoo
tutajitahidi kurekebisha’’alisema Ndalichako
Aidha
Ndalichako aliwaasa wanafunzi katika shule zote alizotembelea wilayani
humo kuacha kuchanganya mambo na kuendekeza kwenye ngoma,muziki au
kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi kwani mambo hayo yanachangia kwa
kiasi kikubwa wanafunzi kufeli.
Kwa
upande wa Mchengerwa aliwataka wanafunzi kujibidiisha na masomo kwa
kuwa katika kipindi cha uongozi wake anajitahidi kuishawishi serikali
kuboresha elimu katika wilaya hiyo ili waweze kuzalisha wasomi wengi
ambao kwa pamoja wataweza kuendeleza wilaya yao.
‘’Naombeni mshikilie elimu msome sana kwani nimejitahidi kuisukuma serikali na hatimaye waziri
amekuja kuona changamoto zetu na kuzitaftia ufumbuzi ,tusirudi nyuma
tunatakiwa kuzalisha maprofesa wengi ambao tutashirikiana kuijenga
Rufiji mpya’’alisema Mchengerwa
Hata
hivyo Mchengerwa aliipongeza serikali kwa kusajili Shule ya Umwe ambayo
wanafunzi walikuwa wanapata shida kusoma shule mbili tofauti kwa kuwa
hawakuruhusiwa kufanya mitihani yao katika shule ambayo haijasaliwa na
kwamba kilichobaki ni mkuboresha miundombinu ya shule hiyo.



No comments
Post a Comment