Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, February 28, 2017

Wanawake 2 kushtakiwa kwa muaji ya Kim Jong nam

Doan Thi Huong, mwenye umri wa 28, kutoka Vietnam na Siti Aisyah, mwenye umri wa 25, kutoka Indonesia

Doan Thi Huong                                                             Vietnam na Siti Aisyah
Mwanasheria mkuu wa Malaysia, anasema wanawake wawili wanaodaiwa kumuua ndugu wa kambo wa rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un watashtakiwa kwa makosa ya mauaji.
Wawili hao, raia wa Indonesia na Vietnam wanakabiliwa na hukumu ya kifo, kwa mauji ya Kim Jong Nam katika uwanja wa ndege mjini Kuala Lumpar.
Malaysia inasema, Bwana Kim aliyekuwa mkosoaji wa nduguye, aliuwawa kwa kutumia sumu aina ya , VX, ambayo imepigwa marufuku na Umoja wa mataifa.
Washukiwa hao wawili wanadaiwa kumpaka usoni kemikali hiyo ya sumu katika uanjwa wa ndege wa Malaysia mapema mwezi huu.
Wamesema kuwa walidhani walikuwa wakifanya mzaha katika filamu.
Watashtakiwa chini ya sheria ambapo iwapo watapatikana na hatia watanyongwa.
Hatahivyo hakuna hatua iliochukuliwa kuhusiana na kumshataki raia wa Korea Kaskazini ambaye pia anazuiliwa kwa muaji hayo.
Wanawake hao ni Doan Thi Huong, mwenye umri wa 28, kutoka Vietnam na Siti Aisyah, mwenye umri wa 25, kutoka Indonesia na ni miongoni mwa washukiwa 10 waliotambuliwa na Malaysia kwamba huenda walihusika na mauaji hayo.
Washukiwa hao ni pamoja na afisa mkuu katika ubalozi wa Korea Kaskazini mjini Kuala Lumpur pamoja na mfanyikazi mmoja wa kampuni ya ndege ya taifa hilo.
Korea Kusini inaamini kwamba washukiwa wanne ni wapelelezi wa Korea Kaskazini.
Chanzo: BBC Swahili
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment