Writen by
sadataley
12:05 PM
-
0
Comments

Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa
Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na
Rais wa Chad, Mhe. Jenerali Idrissa Deby Itno katika Ikulu ya nchi hiyo
jijini N'Djamena, Chad.
Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa
Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na
Rais wa Chad, Mhe. Jenerali Idrissa Deby Itno katika Ikulu ya nchi hiyo
jijini N'Djamena, Chad.
Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa
Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa
na Mwenyekiti Mpya wa Kamisheni Umoja wa Afrika na Aliyekuwa Waziri wa
Mambo ya Nje wa Chad Mhe Moussa Fakhi nyumbani kwake jijini N'Djamena
Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa
Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika
mazungumzo na Mwenyekiti Mpya wa Kamisheni Umoja wa Afrika Mhe Moussa
Fakhi nyumbani kwake jijini N'Djamena
Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa
Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa
na Mwenyekiti Mpya wa Kamisheni Umoja wa Afrika Mhe Moussa Fakhi
nyumbani kwake jijini N'Djamena.
Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa
Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jana tarehe
20 Februari 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Chad, Mhe.
Jenerali Idrissa Deby Itno katika Ikulu yake jijini N'Djamena, Chad.
Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Waziri wa Elimu wa Chad Mhe. Ahmat
Ghazali Acyl na Waziri wa Fedha Mhe. Diguimbaye Christian.
Ziara hiyo ya Rais Mstaafu nchini Chad
ni muendelezo wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu ya kuwafikia viongozi
wa nchi 14 za Afrika za kipaumbele katika kutekeleza mapendekezo ya
Ripoti ya Kizazi cha Elimu (The Learning Generation).
Katika mazungumzo yao, Rais Mstaafu Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Deby wamezungumzia janga
kubwa linaloinyemelea dunia na hasa nchi za uchumi wa kati na chini
ikiwa hakutafanyika mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu.
Viongozi hao wamezungumzia haja ya nchi
za bara la Afrika kuchukua hatua z amakusudi kufanya maboresho na
mageuzi makubwa katika sekta ya elimu katika nchi zao ili kuweza
kuendana na kasi ya nchi zilizoendelea. Azma hiyo inatokana na stadi
kuwa nchi za uchumi wa kati na chini zko nyuma kielimu kwa miaka 50 hadi
70. Aidha, lipo tishio kuwa ifikapo mwaka 2050, kazi na ajira takribani
bilioni 2 zitakuwa zimefutwa kutokana na maendeleo na matumizi ya
teknolojia (automation).
Rais Deby amemuhakikishia Rais Mstaafu
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete uthabiti wa azma ya nchi yake kufanya mageuzi
makubwa katika sekta ya elimu. Ameelezea utayari wa nchi yake kujiunga
na mpango huo wa kufanikisha mapinduzi ya sekta ya elimu ndani ya kizazi
kimoja ifikapo mwaka 2040.
Mbali na mkutano wake na Rais wa Chad,
Rais Mstaafu amekutana pia na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mpya wa
Kamisheni Umoja wa Afrika na Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad
Mhe Moussa Fakhi nyumbani kwake N'Djamena. Rais Mstaafu amempongeza Mhe.
Fakhi kwa kuchaguliwa na Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika kuwa
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja huo na kumtakia kila la kheri katika
majukumu yake mapya. Viongozi hao wawili wamekuwa pia na mazungumzo
yaliyohusu mipango ya Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu barani Afrika na
masuala ya hali ya usalama ya Libya.
Chanzo: Mjengwa Blog
No comments
Post a Comment