Writen by
sadataley
12:08 PM
-
0
Comments
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz P. Mlima, akifungua Mkutano
cha Makatibu Wakuu nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa Kamati Ndogo
ya Mawaziri ya Siasa na Diplomasia ya SADC (Inter State Politics and
Diplomacy Sub Committee-ISPDC) unaotarajiwa kufanyika tarehe 23 na 24
Februari, 2017. Mkutano wa Makatibu Wakuu unafanyika kwa siku mbili
katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es
Salaam.
Sehemu ya wajumbe wa Mkutano kutoka katika mataifa ya nchi wanachama wakifuatilia mkutano.
Kaimu Mkuu wa Mabalozi Mhe. Balozi Edzai Chimonyo (wa kwanza kushoto) na wajumbe wengine wakifuatilia mkutano.
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. Stergomena Tax (wa pili kushoto) na wa
kwanza kulia ni Balozi Simba Yahya, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi wakifuatilia mkutano.
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia Mkutano.
No comments
Post a Comment