UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

Saturday, February 25, 2017

MAWAZIRI WA SMZ WATEMBELEA WIZARA YA ARDHI


LUK1
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akiwaelezea Mawaziri kutoka Zanzibar jinsi Kituo cha Huduma kwa Mteja cha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kinavyorahisisha kutoa Huduma za Ardhi bila usumbufu kwa Wananchi. Kuanzia Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud, Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe. Hamad Rashid, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Zanzibar Mhe. Salama Talib na Katibu Mkuu Wizara wa Ardhi Dkt. Yamungu Kayandabila.
LUK2
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud jinsi ya kutumia mashine ya kutolea huduma za Ardhi katika kituo cha Huduma kwa Mteja cha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
LUK3
Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Zanzibar Mhe. Salama Talib akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi jinsi Wizara yake ilivyofanikiwa kuyapatia ufumbuzi masuala mbalimbali ya Ardhi na kuwaondolea usumbufu Wananchi katika kupata huduma za Ardhi. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara wa Ardhi Dkt. Yamungu Kayandabila.
LUK4
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akiwa na ujumbe wa  Mawaziri kutoka Zanzibar walipofika ofisini kwake.
LUK5
  Wananchi wakipata Huduma za Ardhi katika Kituo cha Huduma kwa Mteja cha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment