Writen by
sadataley
12:23 PM
-
0
Comments
Afisa habari wa habari wa klabu ya Simba Haji Manara ame-post kwenye
ukurasa wake wa Instagram kuhusu mchezaji wao wa zamani Hassan Ramadhani
Kessy na hali anayopitia kwenye klabu yake mpya ya Yanga.
Manara ameandika ujumbe unaosomeka: “Unakumbuka yale maneno ya
aliotudhalilisha huyo dogo? Mwambieni this is Simba na benchi ndio
makazi yako ya kudumu.”
Kessy aliondoka Simba mwishoni mwa msimu uliopita huku usajili wake
ukizua utata mkubwa kati ya vilabu hivyo viwili vyenye nguvu kwenye soka
la Bongo.
Simba wanalalamika kwamba, Yanga ilimsajili Kessy akiwa bado anamkataba
na Simba hali iliyopelekea kufungua kesi TFF ambao baadae Yanga
ilitakiwa kuilipa Simba zaidi ya milioni 50 baada ya kubainika kuvunja
kanuni za usajili wakati wa kumsajili mlinzi huyo wa kulia.
Tangu Kessy ajiunge na Yanga ameshindwa kupata nafasi ya kudumu kwenye
kikosi cha kwanza cha Yanga kwa kumtoa Juma Abdul kwenye nafasi yake.
No comments
Post a Comment