Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Saturday, November 1, 2014

Jeshi lagawanyika kuhusu uongozi B.Faso

   
Kanali Zida asema yeye ndiye anayefaa kuchyukua uongozi.
Mgawanyiko umeripotiwa ndani ya jeshi la Burkina Faso kuhusu ni nani anayefaa kuliongoza taifa hilo kufuatia kujiuzulu kwa rais Blaise Campaore baada ya miaka 27 uongozini.
Kituo kimoja cha radio kilitangaza taarifa kutoka kwa naibu mkuu wa kikosi cha kumlinda rais kanali Isaac Zida iliyosema kuwa amechukua jukumu la kuliongoza taifa hilo.
Mapema mkuu wa majeshi Honore Traore alitangaza kuwa alikuwa amechukua usukani
Jen.Honore Traore
Blaise Compaore alijiuzulu baada ya kushuhudia maandamano yenye ghasia baada ya jitihada zake za kutaka kuliongoza taifa hilo kwa awamu nyengine kupitia bunge kugonga mwamba.
Akizungumza hapo jana kanali Zida amesema kuwa Jenerali Traore hawezi kuliongoza taifa hilo.
''Nimechukua jukumu la kuliongoza taifa hili na serikali ya mpito ili kuliendeleza na kuhakikisha kuwa kuna mabadiliko ya kidemokrasia kwa njia ya amani'' alisema kanali Zida katika hotuba yake katika runinga.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment