Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, November 2, 2014

Watu wa Beni, DRC, waandamana

     Rais Kabila akiwa Beni
Ripoti zinasema kuwa maandamano yamefanywa katika mji wa Beni, mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, baada ya mauaji ya karibuni yaliyofanywa na wapiganaji.
Kituo cha redio cha huko kinasema kuwa waandamanaji wanaodai ulinzi zaidi, wameshambulia sanamu ya Rais Joseph Kabila saa chache baada ya kujulikana kuwa watu 7 zaidi waliuwawa Jumamosi usiku.
Inakisiwa kuwa watu kama 100 wameuwawa katika eneo la Beni katika mwezi uliopita.
Wanaoshukiwa kufanya hayo ni wapiganaji wa ADF - kundi la wapiganaji Waislamu kutoka Uganda ambao sasa wanapigana na jeshi la Congo na askari wa Umoja wa Mataifa.
Alipozuru mji wa Beni Ijumaa, Rais Kabila aliahidi ulinzi zaidi kwa raia na aliomba kuwa kikosi cha Umoja wa Mataifa huko kizidishwe.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment