Writen by
sadataley
5:05 PM
-
0
Comments
Na Julieth Kulangwa
Dar es Salaam. Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amesema katika kipindi cha miaka 10 alichoshikilia nafasi hiyo ya mtendaji mkuu wa Serikali, hatasahau mambo matano makubwa aliyokumbana nayo.
Akizungumza na waandishi wa habari wa Mwananchi nyumbani kwake, Kiluvya, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Sumaye aliutaja uamuzi wa kuvunja Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam na kuunda Tume iliyokuwa chini ya Charles Keenja na kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuwa miongoni mwa mambo hayo.
Sumaye, ambaye alishikilia nafasi hiyo kuanzia mwaka 1995 hadi 2005, alisema kuna mambo mengi aliyokutana nayo wakati akiwa Waziri Mkuu, lakini hayo matano ni makubwa ambayo hatayasahau.
“Katika nchi ya kimaskini kama Tanzania, huwezi kuiongoza kwa miaka 10 bila kufanya jambo ambalo litakufanya ulikumbuke kwa ubaya au uzuri,” alisema na kuongeza:
“Uamuzi mgumu wa kwanza kuufanya ambao kamwe sitausahau ni wa kuvunja Jiji la Dar es Salaam. Wakati tunaingia madarakani Jiji la Dar es Salaam lilikuwa limeoza kabisa kwa uchafu nikasema hapana lazima nifanye kitu.”
Alisema kama kioo cha nchi, Dar es Salaam haikustahili kuwa chafu kiasi kile kwa sababu wageni wote ndiko wanakofikia hivyo ni aibu kwamba katikati ya jiji kulikuwa na hali mbaya ya usafi.
Alisema uamuzi huo ulikuwa mgumu kwa sababu ulihusisha kuondoa viongozi ambao walichaguliwa na wananchi na kuweka uongozi wa kuteuliwa, jambo ambalo ni kinyume na misingi ya kidemokrasia... “Nilikutana na madiwani, wao nikawaambia lazima jiji liwe safi la sivyo tutachukua hatua. Kweli mwaka 1996 ikabidi nivunje jiji,” alisema.
Alisema wengi hawaelewi maana ya kuvunja jiji, “Unaweza kusema (kuvunja jijini) kunapingana na utawala bora, lakini inapobidi kiongozi aokoe jahazi kwa kuwaondoa watu ambao wamechaguliwa na wananchi, ni lazima ifanyike,” aliongeza.
“Nilivunja jiji nikaweka tume ambayo kwa kweli ilifanya kazi nzuri sana. Nakumbuka kabla ya tume hiyo jiji lilikuwa linakusanya kama Sh900 milioni, lakini baada ya kuvunja makusanyo yalipanda mpaka Sh9 bilioni.
“Mji ulikuwa kama hauna shule, lakini zilijengwa na idadi ya watoto kwa darasa ikapungua sana. Wakati ule ilikuwa watoto 140 kwa darasa moja, lakini tumehiyo ilifika mpaka watoto 50 kwa darasa.”
Tume hiyo ya Keenja ambayo ilifanya kazi kubwa ya kuweka taratibu, kusafisha jiji kwa kuondoa mabanda mengi machafu na kufungua barabara zilizokuwa zimefungwa kwa ajili ya ujenzi wa majengo.
Mbunge huyo wa zamani wa Hanang, ambaye anasimulia kwamba alikwenda shule kwa kulazimishwa kutokana na jamii yao kutojali elimu, alisema uamuzi wa pili mgumu ulikuwa ni kuanzisha Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) uliokuwa wa miaka mitano (2002-2006) na ambao ulitumia fedha nyingi.
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Sumaye--Sitasahau-mambo-matano/-/1597296/2455206/-/5ckx2r/-/index.html
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Sumaye--Sitasahau-mambo-matano/-/1597296/2455206/-/5ckx2r/-/index.html
No comments
Post a Comment