Writen by
sadataley
5:08 PM
-
0
Comments
Na Mwandishi wetu, Mwananchi
Mwanza. Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini amesema Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea halina maana yoyote hivyo liachwe limalize muda wake.
Akizungumza kwenye mahojiano jana, Askofu Kilaini alisema mpaka sasa malengo ya Bunge hilo hayajajulikana, hivyo hakuna haja ya wananchi kulumbana na wajumbe hao kwa sababu fedha zilizotumika hazitarudishwa.
“Kama ni fedha zimeshaliwa nyingi tu siku zilizobaki ni chache, Katiba wanayopitisha ni ya wananchi siyo ya Bunge. Lenyewe (Bunge) linapendekeza tu, hivyo hata wakatengeneza rasimu yao si lazima ipitishwe na wananchi,” alisema Askofu Kilaini na kuongeza:
“Wakiweza kuwafanya wananchi waikubali basi hapo maana yake ni nzuri, kitu ambacho ni kigumu kutokea. Tuwaache wamalize muda wao hakuna sababu ya kuleta vurugu kwa sababu ya hilo.”
Alisema jambo muhimu kwa sasa ni kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa na ule mkuu mwakani uwe wa haki, washiriki waridhike na makubaliano yaliyofikiwa kati ya Rais Kikwete na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) yamesaidia.
“Rais (Jakaya Kikwete) amefanya uamuzi wa busara kuahirisha Bunge Maalumu la Katiba kwa sababu hatima yake haiwezi kupatikana Katiba Mpya kipindi hiki kifupi.
Tumejaribu kipindi cha kwanza lakini ni bora kuruhusu uchaguzi mkuu, hili ni muhimu la kuzingatia. Hatutakuwa wa kwanza kuahirisha mchakato huu kwa sababu Kenya, Afrika Kusini hata Marekani wamefanya hivyo kwa mara nyingi,” alisema Kilaini na kuongeza:
Askofu Kilaini alisema mambo muhimu kwake ni uwapo wa Tume Huru ya Uchaguzi, Mgombea binafsi ingawa kwa sasa kushinda urais itakuwa ni vigumu.
No comments
Post a Comment