Writen by
sadataley
5:26 PM
-
0
Comments
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Cillin Frisch (kulia)
akimsindikiza aliyekuwa kocha wa klabu hiyo, Zdravko Logarusic baada ya
mkataba wake kusitishwa na Kamati ya Utendaji ya Simba iliyokutana jana.
Picha na Michael Matemanga.
Na Khatimu Naheka na Sosthenes Nyoni, MwanachiDar. Ajira ya aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba Zdravko Logarusic
imefikia tamati rasmi jana baada ya uongozi wa klabu hiyo kusitisha
mkataba wake.
Logarusic, maarufu kwa jina la Loga alisaini
mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha Simba mwezi uliopita, ikiwa ni hatua
ya kuongeza ule wa miezi sita ambao aliusaini Desemba mwaka jana wakati
akichukua nafasi ya wazawa Abdallah Kibaden ‘King’ na Jamhuri Kihwelo
‘Julio’.
Akitangaza uamuzi huo katika mkutano mfupi
uliotumia dakika tano tu kwenye Hoteli ya Serena, Rais wa Simba, Evans
Aveva alisema wamelazimika kusitisha mkataba na Loga kwa sababu ya hulka
na tabia ya mwenendo wa kocha huyo kushindwa kuendana na ule wa Simba.
Aveva alisema kabla ya kufikia uamuzi huo, uongozi
wake ulikuwa na vikao vingi na Loga vikimtaka kubadilika kila anapokuwa
anaonyesha toafuti, lakini ilishindikana.
“Kutokana na hilo leo (jana) asubuhi, niliitisha
kikao cha Kamati ya Utendaji kujadili tatizo hilo na tukakubaliana
kufanya uamuzi huo, lengo likiwa kuinusuru klabu yetu,” alisema Aveva.
“Tulikutana na kocha mwenyewe baada ya mimi na
kamati yangu kuona tuchukue uamuzi huo na hata yeye mwenyewe
alikubaliana na hilo kwamba ni vyema tukaachana kwa hali ya amani.
“Niwahakikishie Wanasimba kuwa uamuzi huu
tumeuchukua baada ya kufanya tafakuri ya kina na haya yote tunayafanya
ikiwa ni kuzidi kubeba dhamana, ambayo wametupa mimi na kamati yangu ya
utendaji kwa ajili ya mafanikio ya klabu yetu ya Simba na tunamshukuru
na kumtakia kila la kheri kocha Logarusic.
Juzi baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Simba
na Zesco ambao Wekundu hao walilala kwa mabao 3-0, ilibainika kuwa Loga
alikuwa mkali kwa baadhi ya wachezaji wake na kuwatolea lugha kali, huku
akitangaza kwamba baadhi yao hataki kuingia nao kambini.
“Ni kweli nilikuwa mkali kwa baadhi ya wachezaji
baada ya mchezo, mimi ni kocha na Simba ilinikabidhi jukumu la kuongoza
timu, huku uongozi ukiangalia utawala, siwezi kuwa na furaha na mchezaji
ambaye hataki kufuata kutekeleza,”alisema Loga saa chache kabla ya
kufutwa kazi.
Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Simba
kimeliambia gazeti hili kuwa, Loga ametimuliwa kutokana na kitendo cha
kuwatukana wachezaji akiwatuhumu kuonyesha kiwango duni wakati wa mechi
dhidi ya Zesco.
“Ebu fikiria ilifikia hatua ya kuwaambia wachezaji
waliokuwa timu ya taifa kwamba hawana msaada, aliwambia Kiemba (Amri)
na Uhuru (Selemani) watafute timu ya kwenda kwa mkopo hataki kuwaona,
huyu kocha anafaa kweli,” kilieleza chanzo hicho.
“Tulimvumilia sana kwa sababu wachezaji walikuwa
wanalalamika kutukanwa na wakati mwingine kwa jambo dogo la kumwelekeza
mchezaji, hakufanya hivyo zaidi ya kufoka.”
Kufuatia kuondoka kwa Loga, taarifa za kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa tayari Wekundu hao wameanza mazungumzo na Kocha Mzambia, Patrick Phiri ambaye ndiye anapewa nafasi kubwa ya kuchukua timu.
Kufuatia kuondoka kwa Loga, taarifa za kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa tayari Wekundu hao wameanza mazungumzo na Kocha Mzambia, Patrick Phiri ambaye ndiye anapewa nafasi kubwa ya kuchukua timu.
No comments
Post a Comment