Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, July 19, 2014

Ukawa washikilia msimamo wao


Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakijadiliana jambo. Picha na Maktaba 
Na Ibrahim Yamola, MwananchiDar es Salaam. Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umeshikilia msimamo wake kuwa uko tayari kufanya mazungumzo ya kumaliza mpasuko uliojitokeza katika Bunge Maalumu la Katiba na siyo kurudi bungeni.
Pia umesema kwamba hawatashiriki Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 endapo Katiba Mpya haitapatikana au iliyopo haitafanyiwa marekebisho.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Ukawa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa Kamati Kuu ya Chama hicho.
“Ukawa hatuwezi kukataa mazungumzo ya kutafuta mwafaka na faida kwa Watanzania lakini tunaweza kukataa kurudi bungeni endapo kile kilichotufikisha hapa na nini kilisababisha hakijapata ufumbuzi.
Mbowe alisema Rais Jakaya Kikwete kwa mujibu wa sheria ndiye mwenye uwezo wa kuufanya mchakato huu ukamalizika salama na ikapatikana Katiba yenye kujali masilahi ya wananchi wote.
“Tunamtaka Rais (Kikwete) tunakwenda katika majadiliano aache kuwa kigeugeu na asimame kama kiongozi wa wananchi ili amalize uongozi wake salama na kuiacha nchi katika amani kama alivyoikuta,” alisema Mbowe.
Hivi karibuni katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema Ukawa wako tayari kurejea bungeni hata usiku wa manane endapo watahakikishiwa kuwa mjadala wa Bunge hilo utajikita katika rasimu iliyopo mezani.
“Sisi Ukawa tuko tayari kurejea bungeni hata saa nane za usiku ila wakituhakikishia tunakwenda kujadili Rasimu iliyobeba maoni ya Watanzania kinyume na hapo hatutakubali kurejea,” alisema Dk Slaa.
Alisisitiza kwamba “Hata kama tutarejea bungeni, yakitokea yaliyotufanya tutoke, tutachukua uamuzi haraka.”
Alisema CCM haina nia ya kupatikana kwa Katiba Mpya na imekuwa ikitumia nguvu kutaka kuuharibu ili Katiba hii iliyopo iendelee kutumika.
“Tuna ushahidi wa sauti ya Kamati Kuu ya CCM iliyokaa hivi karibuni wakionyesha kutokuwa na dhamira ya kweli ya kuipatia nchi hii Katiba na muda utakapofika tutauweka wazi ili Watanzania wauone na wausikie,” alisema Mbowe.
Ukawa unaoundwa na vyama vya siasa vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi vilisusa na kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge Aprili 16 mwaka huu kwa madai ya kuwa zipo dalili za kutaka kuichakachua Rasimu ya Katiba iliyosheheni maoni na mapendekezo ya wananchi.
Kufuatia mpasuko huo na Agosti 5 mwaka huu Bunge hilo likitarajia kukutana kwa siku 60, Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta ameteua wajumbe 30 wa kamati ya mashauriano inayotarajia kukutana Julai 24 mwaka huu.
Kuhusu Uchaguzi Mkuu ujao mwakani, Mbowe alisema, “Kama Katiba haitapatikana na ikabaki hii hii....Hatuwezi kuingia katika uchaguzi kwa kutumia katiba ya sasa ambayo inaonyesha kuwapo kwa tume huru ya uchaguzi kumbe siyo kweli.”
Naye Mjumbe Kamati Kuu ya Chadema na aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu alisema, “tukijidanganya nchi hii ikishindwa kupata Katiba Mpya itakuwa ni upumbavu.”
Alisema: “Kilichowatokea majirani zetu Kenya kinaweza kikatokea hata hapa kwetu, busara na hekima inatakiwa itawale ili mchakato huu umalizike salama.”
Profesa Baregu alisema “Rais (Kikwete) inabidi avue koti lake la uanachama wa CCM kama Mwenyekiti ana avae joho la urais.”
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment