Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, July 19, 2014

Butiku aionya CCM


Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku  
Na Exuper Kachenje, Mwananchi
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amekionya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwa kipo hatarini kupoteza madaraka katika uchaguzi mkuu ujao, iwapo kitafanya makosa na kuendekeza ubinafsi na utawala wa kiimla unaotokana na utamaduni wa rushwa na matumizi mabaya ya mali za umma.
Butiku ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alisema kuwa iwapo chama hicho kitasahau kuwa kinaiongoza nchi kwa mujibu wa Katiba ya nchi ambayo sasa Watanzania wanataka iandikwe upya na kuendelea kukumbatia maovu kinaweza kuondolewa madarakani.
Alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam, Jumatano wiki hii katika mahojiano maalumu na gazeti hili ambapo alizungumzia mambo mbalimbali.
“…Kosa moja la msingi ni CCM kusahau misingi ya Katiba ya chama chao na Katiba ya nchi. Watanzania wengi wanaikubali Katiba ya CCM na Katiba ya nchi, lakini ambayo wanasema itazamwe upya, iandikwe Katiba Mpya,” alisema Butiku.
Huku akisisitiza, Butiku alisema: “CCM wakisahau kwamba madaraka yao ni ya kikatiba, wakadhani yapo katika utawala wa kiimla unaotokana na kuimarisha utamaduni wa rushwa na matumizi mabaya ya mali na rasilimali za taifa, watapoteza madaraka kama siyo leo ni kesho.”
Alifafanua kuwa hali hiyo itaikumba CCM kwa kuwa ndiyo kanuni ya maisha ya binadamu akisema:
“Vyama vyote tawala vilivyosahau masilahi ya wananchi wake, demokrasia, uhuru na haki, vikakumbatia uovu vinaanguka. Huo siyo utabiri wangu binafsi, bali historia itawahukumu.”
Butiku alitoa mfano akieleza: “Mfumo wa kibabe zaidi wa makaburu wa Afrika Kusini, uliangushwa na wasio na viatu. Nani anaweza kujenga ubabe wa sura kama ule wa makaburu, nani ataruhusu? Ni muhimu CCM nayo ijitazame.”
Rushwa
Alisema kuwa alipoondoka madarakani, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alisema taifa linanuka rushwa hali ambayo imeota mizizi hata sasa.
“…Leo rushwa ni kawaida, ni mfumo wa kuuza na kununua uongozi, kama taifa mkifika hapo ni hatari. Mkishanunua uongozi basi mmekwisha. Mkijenga mfumo huo, mnaondoa haki.
Ikiwa kura yako imekuwa biashara umekwisha, hakuna ushirikiano tena kati ya kiongozi aliyenunua nafasi na mwananchi. Hapo mnajenga kundi la viongozi la wafanyabiashara wa kura katika uchaguzi, mnajenga mfumo wa raia kuwa maskini.”

“Raia wakiuza haki yao na kununua hakutakuwa na taifa lenye utulivu. Wanunua kura wajue ni vita, siku moja wauza kura wataamua kuwaondoa nao watagoma kwa kuwa walinunua uongozi, hapo damu itamwagika, watu watauana.
Wanyonge hawapotezi haki ya unyonge wao, unaweza kuiangusha CCM…
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment