Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, July 17, 2014

Matokeo kidato cha sita yatia fora


Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) Dk Charles E. Msonde  
Na Ibrahim Yamola, MwananchiDar es Salaam. Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka 2014 ambayo yanaonyesha kupanda kwa kiasi kikubwa cha ufaulu kutoka asilimia 87.85 mwaka 2013 na hadi 95.98 mwaka huu.
Katika matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Necta, orodha ya kumi bora imetawaliwa na shule nyingi zenye majina yasiyo maarufu, huku shule maarufu ya sekondari ya Tambaza na ya Ufundi ya Iyunga zikiwa miongoni mwa shule 10 zilizoshika mkia.
Hata hivyo, ufaulu wa mwaka huu unaonekana kuchangiwa na idadi ndogo ya watahiniwa kulinganisha na mwaka jana, hali ambayo imejionyesha pia kwenye idadi ya wanafunzi waliohusika na udanganyifu ambao mwaka huu ni wawili tofauti na wanne wa mwaka jana.
“Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kutumia fursa hii kuzipongeza Kamati za Uendeshaji Mitihani za Mikoa na Wilaya, wakuu wa shule na wasimamizi wa mtihani uliofanyika Mei, 2014 kwa kuzingatia na kusimamia taratibu za uendeshaji mitihani na hivyo kuzuia udanganyifu kufanyika,” alisema kaimu katibu mtendaji wa Necta, Dk Charles E. Msonde wakati alipozungumza na waandishi wa habari jana.
“Aidha Baraza linawapongeza watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha sita 2014 kwa kutojihusisha na udanganyifu,” aliongeza katibu huyo ambaye alijikita katika taarifa aliyoiandaa kutangaza matokeo hayo.
Mwaka huu waliofanya mtihani walikuwa 40,695 na waliofaulu ni 38,905 ambao ni sawa na asilimia 95.98, wakati mwaka 2013 watahiniwa waliofanya mtihani walikuwa 50,611 na waliofaulu walikuwa 44,366 sawa na asilimia 87.85.
Katika matokeo hayo, wavulana wameendelea kufanya vizuri katika masomo ya sayansi huku wasichana wakifanya vyema katika masomo ya lugha na biashara.
Dk Msonde alisema ufaulu wa mitihani umeimarika ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Watahiniwa wa shule, kati ya 35,650 waliosajiliwa ni 35,418, sawa na asilimia 99.35, walifanya mtihani. Wasichana walikuwa 11,022 sawa na asilimia 99.63 na wavulana walikuwa 24,396, sawa na asilimia 99.22.
Dk Msonde alisema watahiniwa wa kujitegemea waliosajiliwa walikuwa 6,318. Kati yao, watahiniwa 5,277 (asilimia 83.52) walifanya mtihani na watahiniwa 1,041 (asilimia 16.48) hawakufanya mtihani.
“Jumla ya wasichana waliofaulu ni 12,080 sawa na asilimia 97.66 wakati wavulana ni 26,825 sawa na asilimia 95.25 ya watahiniwa wote 38,905 waliofanya mtihani,” alisema Dk Msonde.
“Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonyesha jumla ya watahiniwa 30,225 sawa na asilimia 85.73 wamefaulu katika madaraja I-III wakiwamo wasichana 9,954 sawa na asilimia 90.59 na wavulana 20,271 sawa na asilimia 83.53.”
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Matokeo-kidato-cha-sita-yatia-fora/-/1597296/2386998/-/11hwq0oz/-/index.html
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment