Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, July 17, 2014

Tido Mhando aaga Mwananchi

Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited (MCL), Tido Mhando akizungumza na wafanyakazi wa MCL jijini Dar es Salaam jana. Picha na Venance Nestory 
Na Mwandishi Wetu, MwananchiDar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Tido Mhando amewaaga wafanyakazi wa kampuni hiyo baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka miwili na nusu.
Mkataba wa Tido katika kampuni ya Mwananchi utafika kikomo mwishoni mwa mwezi huu.
Taarifa ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Nation Media Group (NMG), Linus Gitahi kwa wafanyakazi wote wa Afrika Mashariki ambako kampuni hiyo inamiliki vyombo vya habari, inasema Mhando anaondoka MCL huku akiacha mafanikio makubwa katika nyanja zote na kwamba atakumbukwa kwa mchango wake.
MCL ni kampuni tanzu ya NMG inayochapicha magazeti ya Mwananchi, Mwananchi Jumamosi, Mwananchi Jumapili, The Citizen, The Citizen on Saturday, Sunday Citizen na Mwanaspoti.
Kabla ya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MCL mwaka 2012, Mhando alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kati ya mwaka 2006 na 2010. Awali alikuwa Mkuu wa Idara ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la BBC (1999-2006).
Mhando aliiwezesha MCL kukua kwa kasi kubwa katika mapato na katika mpango wa uchapishaji wa magazeti ya MCL Kanda ya Ziwa ambako wakazi wa mikoa hiyo sasa wamekuwa wakisoma magazeti asubuhi tofauti na zamani.
Wafanyakazi wa MCL walimpongeza kwa kuboresha masilahi yao kwa kipindi cha uongozi wake na kuandaa misingi bora ya uongozi, ikiwamo kumwandaa mrithi wake.
Akiwaaga wafanyakazi jana asubuhi, Mhando aliwashukuru kwa ushirikiano wao pia alisema amejifunza mambo mengi mapya, ikizingatiwa kuwa kwa miaka mingi alikuwa kwenye sekta ya habari ya utangazaji tofauti na uchapishaji. “Safari hii ilinipa uzoefu mpya na wenye changamoto nyingi lakini kupitia ushirikiano wenu wa dhati tulifanikiwa kuiweka kampuni katika hali nzuri,” alisema Mhando.
Gitahi alisema nafasi ya Mhando itachukuliwa na aliyekuwa Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa MCL (COO), Francis Nanai.
Nanai alijiunga MCL , Agosti mwaka jana akitokea Kampuni ya Saruji ya Mbeya Cement (Lafarge Tanzania) ya mkoani Mbeya akiwa Mkurugenzi wa Biashara.
Frederick Sumaye akihutubia TYDC Mwanza
  • Wapinzani washtukia ziara yake
ZIARA ya Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, imeacha wimbi la hofu ya kisiasa miongoni mwa viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani mkoani Mwanza.
Sumaye, mmoja wa wanasiasa wanaotajwa kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, alifanya ziara ya siku nne mkoani hapa, wiki iliyopita.
Pamoja na mambo mengine, Sumaye alitumia fursa hiyo kuzindua Taasisi ya Maendeleo ya Vijana Tanzania (TYDC) Tawi la Mwanza.
Mara zote alipopata fursa ya kuhutubia katika mikutano ya vijana kwa nyakati tofauti jijini hapa, Sumaye alisema hana lengo la kutafuta umaarufu wa kisiasa kama ambavyo inaweza kudhaniwa na baadhi ya watu.
Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani mkoani Mwanza wameeleza kuishtukia ziara hiyo ya Sumaye wakiihusisha na mkakati maalum  wa kujinyooshea mapito kuelekea Uchaguzi Mkuu mwakani.
Katika mahojiano maalum na Raia Mwema jijini Mwanza juzi, Katibu wa Ofisi ya Mbunge wa Nyamagana, Mwinamila Robert (CHADEMA), amesema Sumaye anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa kigezo cha kuhamasisha maendeleo ya vijana na mapambano dhidi ya maovu nchini.
“Katika hili dhamira ya Sumaye lazima itakuwa ya kujijenga kisiasa miongoni mwa vijana, hasa kwa kuzingatia kuwa ameshatangaza nia yake ya kuutaka urais,” amesema Mwinamila na kuendelea:
“Ziara hiyo ya Sumaye ilikuwa ni mwavuli tu na kiini macho, na anafanya hivyo baada ya kubaini kwamba wapigakura wengi siku hizi ni vijana, ndiyo maana anajitahidi kuwa karibu na vijana.
“Sumaye kusema kwamba anachokifanya ni kuhamasisha maendeleo ya vijana na mapambano dhidi ya vitendo vya uhalifu ni danganya toto tu, mimi ninaamini dhamira yake imejikita katika kutafuta umaarufu wa kisiasa.”
Mtazamo huo wa Mwinamila pia unamhusisha Sumaye na mkakati wa kuwagawa vijana kutokana na kuelekeza nguvu kubwa zaidi kwa vijana ambao ni wanachama wa CCM.
“Mimi nasema ziara ya Sumaye hapa Mwanza pia ina picha ya kuwagawa vijana, kwa sababu ukiangalia vijana wengi waliohudhuria makongamano aliyohutubia ni wanachama wa CCM, na hata watu walioalika mikutano hiyo ni viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).
“Sasa kwa utaratibu huo, unadhani anawaunganisha vijana? Si kweli, ni dhahiri kuwa anawabagua vijana wa vyama vingine vya siasa na kuwapendelea wa chama chake,” ameseama Mwinamila.
Hata hivyo, hoja ya kwamba Sumaye anawabagua vijana wa vyama vingine vya siasa inakosa nguvu kutokana na ukweli kwamba vijana waliohudhuria makongamano yaliyohutubiwa na kada huyo wa CCM ni wanafunzi wa shule na vyuo mbalimbali visivyokumbatia itikadi ya chama chochote cha siasa.
Kwa upande mwingine, Mwinamila anahofia ziara hiyo ya Sumaye akisema inaweza kuathiri nguvu ya vyama vya upinzani ambavyo vinaendelea na juhudi za kujiimarisha kisiasa mkoani Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa jumla.
“Ziara hiyo ya Sumaye inaweza ikatuathiri sisi wapinzani katika Uchaguzi Mkuu ujao, hasa katika ngazi ya urais, lakini kwenye ngazi ya ubunge na madiwani tuko vizuri,” amesema.
Lakini kwa upande mwingine, Mwinamila anasema vijana na wananchi kwa jumla hawana sababu ya kukataa kupokea fedha zinazoangukia mikononi mwao kutoka kwa wanasiasa wanaotafuta umaarufu wa kisiasa, ilimradi wawe makini kuchagua mtu mwenye uwezo wa kuwaletea maendeleo ya kweli.
“Miminawambia wananchi kwamba kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu kuna watu wanakuja na pesa zao, watu wazichukue tu wale, lakini kwenye uchaguzi wahakikishe wanakuwa makini kuchambua pumba na mchele,” amesisitiza.
Kwa upande wake, Kamishna wa chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) Kanda ya Ziwa, Shabani Itutu, amesema Sumaye hana dhamira ya kweli ya kuhamasisha maendeleo ya vijana nchini bali mlengo wake ni wa kujisafishia njia ya kukubalika wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao.
Itutu ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Uongozi ya ADC Taifa, anasema Sumaye kwa sasa anatekeleza mkakati wake wa kujijenga kwa vijana kwa kuwa ndilo kundi ambalo halina kumbukumbu ya kutosha kuhusu utendaji wake wakati wakiwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Rais Benjamin Mkapa.
“Unajua, Sumaye anachokifanya sasa anadhani kwamba watu wamesahau upungufu ulioonekana katika Serikali ya Awamu ya Tatu, ndiyo maana anaonekana kujikita kwa vijana ambao ni wazi kuwa wengi wao hawana kumbukumbu nzuri ya mambo ya nyuma,” amesema Itutu na kuongeza:
“Hata hiyo kauli ya Sumaye kwamba yuko mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya maovu hapa nchini mimi siiungi mkono kwa sababu ninakumbuka wakati akiwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tatu vitendo vya ujambazi na ufisadi viliongezeka.
“Sasa amepata wapi nguvu ya kupambana na maovu kipindi hiki ambacho yuko nje ya system [serikalini] wakati alipokuwa Waziri Mkuu hakufanikiwa katika mapambano hayo.
“Kwa hiyo, Sumaye kusema kwamba anapambana na maovu si kweli, anawafumba watu, anachotafuta ni umaarufu mwingine wa kisiasa, lakini huo mkakati wake hauwezi kufanikiwa maana watu wengi tunamjua sifa yake.
“Anaweza akaendelea kujifisia kwamba yeye ni mtu bora kuliko wanasiasa wengine hata ndani ya CCM, lakini wananchi wengi tunamfahamu,” amesema Itutu.
Wakati wa ziara yake mkoani Mwanza, Sumaye alipata fursa ya kuhutubia mikutano ya vijana huku akitumia nafasi hiyo pia kukemea watu wakiwamo wanasiasa wanaowatumia vijana kutimiza malengo yao binafsi.
Alisema vijana ni hazina ya taifa yenye nafasi kubwa ya kuijenga nchi katika mazingira ya ustawi wa kiuchumi na kijamii, hivyo wanastahili kupewa fursa za kujijenga kiuchumi badala ya kuwa madaraja ya kuneemesha ‘wajanja’ wachache.
Kwambaa wanasiasa wanapaswa kuwasaidia vijana kutatua matatizo yanayowakabili badala ya kuwatumia kujineemesha na kuwaacha katika hali ya umaskini.
Sumaye alifafanua kuwa vijana ndiyo waathirika wakubwa wa matatizo ya ukosefu wa ajira, vitendo vya rushwa, ufisadi na dawa za kulevya yanayoendelea kushika hatamu hapa nchini.
Huku akijifananisha na askari hodari aliye mstari wa mbele katika kupambana na matatizo hayo kwa kipindi kirefu, Sumaye alisema chanzo cha matatizo hayo ni ukosefu wa uwajibikaji makini wa viongozi na matumizi mabaya ya rasilimali za nchi.
“Mimi niko mstari wa mbele sana kupambana na matatizo haya, sijaanza leo, au kwa mtazamo wa kisiasa, na nitaendelea kupambana, niwe na madaraka, nisiwe na madaraka nitaendelea kupambana na maovu katika nchi hii.
Kwa mujibu wa Sumaye, baadhi ya watu wamekuwa wakitumia fedha nyingi kujipatia umaarufu wa kisiasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu mwakani, huku wakitoa ahadi feki za kuwapatia vijana uongozi.
Aliwaasa vijana kujihadhari na wanasiasa wa aina hiyo kwa manufaa yao na mustakabali wa taifa letu.
Kwa upande mwingine, aliiasa taasisi ya TYDC na vijana kwa jumla kutokubali kufanya fujo na kutumiwa na wanasiasa wanaotaka kutimiza malengo yao ya kisiasa.
“Vijana msiingie katika fujo kwani nchi ikiharibika ninyi ndiyo mtaishi katika uharibifu huo kwa muda mrefu… msiwe sehemu ya kutumika kuliingiza taifa katika majanga.
“Msikubali kudanganywa mkaiharibu nchi yetu kutokana na shida ya muda mfupi, msikubali kujiingiza katika maovu kwa sababu hiyo ni laana ya uhakika,” alisisitiza.
Kuhusu nia ya kugombea urais wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao, Sumaye aliisema yuko tayari kugombea wadhifa huo iwapo ataombwa na wananchi kufanya hivyo.
“Wananchi wakiniomba nitagombea, kwanini nisigombee, nikiombwa nitagombea,” alisema Sumaye wakati akijibu swali la mwandishi aliyetaka kujua msimamo wake kuhusu urais.
Kuhusu idadi kubwa ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaendelea kutangaza nia ya kuomba kuteuliwa na chama hicho kugombea nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu ujao, Sumaye alisema hali hiyo ni ya kawaida, hasa wakati rais anapokaribia kustaafu.
“Rais anapokaribia kuondoka madarakani watu wengi hujitokeza kuwania urais kuliko wakati mwingine, lakini pia sasa hivi kuna mwamko mkubwa wa kisiasa,” aliongeza.
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/sumaye-azua-hofu-ya-kisiasa-mwanza#sthash.4TLqNTxg.dpufZIARA ya Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, imeacha wimbi la hofu ya kisiasa miongoni mwa viChristopher Gamaina...ZIARA ya Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, imeacha wimbi la hofu ya kisiasa miongoni mwa viChristopher Gamaina...

- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/sumaye-azua-hofu-ya-kisiasa-mwanza#sthash.4TLqNTxg.dpuf
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment