Writen by
sadataley
6:50 PM
-
0
Comments
Na Waandishi Wetu, MwananchiDodoma na Dar es Salaam. Kumekuwa na mvutano mkubwa katika vikao vya mashauriano kati ya Serikali na Kamati ya Bunge ya Bajeti, ambao pamoja na mambo mengine unaelezwa kuchangiwa na hatua ya Serikali kukataa kuweka wazi vyanzo vya mapato kwa wajumbe wa kamati hiyo.
Kutokana na hali hiyo, majadiliano kuhusu mwelekeo
wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2014/15, yamejikita katika
makadirio ya matumizi pekee ambayo ni Sh19 trilioni, bila kufafanua
fedha hizo zinatarajiwa kutoka katika vyanzo vipi.
Habari kutoka ndani ya vikao hivyo zinasema
mvutano baina ya timu ya Serikali inayoongozwa na Waziri wa Fedha, Saada
Nkuya Salum kwa upande mmoja na Kamati ya Bajeti inayoongozwa na Mbunge
wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge ni dhahiri hakuna makubaliano
ambayo yamefikiwa hadi sasa.
Wajumbe wa kamati hiyo wamekuwa wakitaka kufahamu
vyanzo vya mapato ili kujiridhisha iwapo Serikali imezingatia ushauri wa
Bunge kuhusu kuongeza vyanzo vipya, badala ya kuongeza kodi katika
vyanzo vilevile kila mwaka.
“Tunashangazwa na makadirio ya matumizi ya Sh19
trilioni kwa mwaka ujao wa fedha wakati wameshindwa (Serikali) kukusanya
Sh18 trilioni na kusababisha upungufu wa fedha katika bajeti ya sasa.
Wakijitahidi watamaliza mwaka huu wa fedha (Juni 30), wakiwa na upungufu
wa zaidi ya Sh600 bilioni, sasa tunataka kujua ni vyanzo gani
vitatumika kupata hizo trilioni 19?”
Chanzo kingine kilisema madai ya wabunge kutaka
kufahamu vyanzo vya mapato yanatokana na kupewa taarifa za siri kwamba
Serikali inakusudia kuongeza kodi katika vyanzo vilevile vya miaka yote,
vikiwamo sigara, mafuta, soda na bia, hali ambayo walihisi kuwa ni
kupigwa teke kwa mapendekezo waliyoyatoa mwanzoni mwa mwaka jana.
Hata hivyo, Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima
alipoulizwa sababu za Serikali kuficha vyanzo vyake kwa wabunge kupitia
ujumbe mfupi wa maandishi ya simu alijibu: “Nashauri swali hilo
lielekezwe kwenye chanzo chako kwa kuwa mimi sina taarifa hizo.”
Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai alisema taarifa
zilizopo ni kwamba Kamati ya Bajeti na Serikali walikuwa wakiendelea na
majadiliano na kwamba vikao husika vitaendelea leo... “Hakuna taarifa
zozote rasmi kutoka ndani ya kikao hicho, tusubiri maana Alhamisi siyo
mbali tutafahamu tu, tuwe na subira.”
Kabla ya kuundwa kwa Kamati ya Bajeti, Chenge
aliongoza Kamati Maalumu iliyoundwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda
kuchunguza mwenendo wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Iliwasilisha
taarifa iliyobaini madudu katika mfumo wa bajeti.
Katika ripoti yake, kamati hiyo ilibainisha kuwapo
kwa udhaifu katika ukusanyaji wa mapato na kwamba kwa mwaka wa fedha
2012/13 pekee, Serikali ilipoteza Sh3.95 trilioni kutokana na kasoro
zilizopo.
Mapendekezo ya Bunge
Ripoti hiyo iliyowasilishwa kwa Spika Makinda
Februari 8, mwaka jana na baadaye kuwasilishwa serikalini, ina
mapendekezo ya vyanzo vipya 24 vya mapato ambayo Chenge alisema kama
yangetekelezwa yangeiwezesha Serikali kupata ziada ya Sh14.86 trilioni
katika bajeti zake za 2014/15 na 2015/16.
Kwa habari zaidi ingia http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Serikali--Bunge-wakabana-koo/-/1597296/2342548/-/7d9p39/-/index.html
Kwa habari zaidi ingia http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Serikali--Bunge-wakabana-koo/-/1597296/2342548/-/7d9p39/-/index.html
No comments
Post a Comment