Writen by
sadataley
6:43 PM
-
0
Comments
Kama ilivyokuwa kwa wiki iliyopita, hii leo tena GK imefanikiwa
kukusanya baadhi ya picha kutoka mikoa mbalimbali kuhusiana na ibada
ambazo zimefanyika siku ya jumapili ya juzi ya tarehe 8. Kwakuanza
kabisa tunaanzia mkoani MBEYA ambako kulifanyika tukio la
kihistoria kwa kijana Caleb Mwanjoka akimshirikisha Robert Mahona katika
kurekodi DVD live iitwayo 'Dhabihu za Sifa' huko mitaa ya RICC Forest
mpya jijini Mbeya, uwepo wa Mungu unaelezwa kuwaatamia watu wake.
|
Caleb Mwanjoka akiwa uweponi. |
|
Caleb akiwa amesujudu uweponi mwa Mungu, hata waitikiaji nao waliguswa kama wanavyoonekana. |
|
Watu wakiwa wanamuabudu Mungu. |
|
Mchungaji Matthew Sasali akizungumza jambo. |
|
Picha ya pamoja baada ya kazi nzito.©Matthew Sasali |
Tukitoka mkoani Mbeya na sasa tunaingia mkoani TANGA ambako tumepata
baadhi ya picha za ibada ya jumapili katika kanisa la Ufufuo na Uzima
linaloongozwa na mchungaji John Kilima, ambapo ilikuwa jumapili ya pekee
watu kula neno la Mungu, pamoja na kipindi cha maombi ya watu
kufunguliwa katika mitego mbalimbali.
|
Mchungaji John Kilima akihubiri. |
|
Mchungaji Kilima akihubiri huku waumini wakimsikiliza. |
|
Watoto wa showers kutoka Ufufuo Tanga wakimsifu Mungu.©Ufufuo crew |
Baada ya kutoka Tanga na sasa tunaelekea kule visiwani, ambako GK
inapicha za ibada ya kusifu na kuabudu kutoka kanisa la TAG Zanzibar
City Centre kwa askofu Kaganga, ambapo ibada hiyo ilijawa na sifa kwa
Mungu, kipindi ambacho kilikuwa kinaongozwa na kundi la Shekina na
waimbaji wengine.
|
Shekina wakimsifu Mungu. |
|
Baadhi ya waumini kama wanavyoonekana.
|
|
Wageni mbalimbali waliofika katika ibada hiyo juzi wakitoa salamu. |
|
Askofu Dickson Kaganga akizungumza katika ibada hiyo©ZanzibarCityCentre |
Baada ya kutoka visiwani Zanzibar, tunamalizia ngwe yetu jijini Dar es
salaam, moja kwa moja mpaka kule Kigamboni ambako kuna kanisa liitwalo
River of life ministries lililochini ya mtume Mary Lutumba ambapo
kumekuwepo na semina mbalimbali za neno la Mungu, na siku ya jumapili
kanisa hilo liliwakumbuka wajane kwa kuwapa zawadi mbalimbali.
|
Mtume Mary Lutumba akihubiri. |
|
Neno lilifundishwa haswa na mtume huyu. |
|
Mtume Lutumba akikabidhi unga kwa mmoja wa wamama hao waliofika kanisani hapo. |
|
Mtume Lutumba akikumbatiana na wamama hao.©Mary Lutumba |
Tukio la mwisho kwa leo ni kutoka usharika wa Kilutheri Mbagala ambako
kulikuwa na ibada safi, huku upande wa sifa na kuabudu uliongozwa na
kundi zima la kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama ambao walikuwa wageni
katika usharika huo siku ya jumapili.
|
Modest Morgan akiliongoza kundi la Kijito katika kumsifu Mungu. |
|
Ngoma wa ngoma ikienda sawa na wana wa Kijito. |
|
Baadhi ya wana Kijito na waumini wa kanisa la Kilutheri Mbagala wakimsifu Mungu©Onai Joseph. |
Habari hii ni kwa hisani ya gospel kitaa
No comments
Post a Comment