Writen by
sadataley
1:37 PM
-
0
Comments
HAPA ILIPOTEMBELEA ZURU SHAMBA LA WAZIRI MKUU PINDA ZUZU DODOMA
Kwaya
maarufu ya Uinjilisti ya KKKT Kihesa mjini Iringa, iko mjini Dodoma
kuchapa Injili ili mataifa waokoke. Kabla ya huduma hiyo muhimu ya
kiroho, jana ilipata fursa ya kuzuru katika shamba la Waziri Mkuu Mhe.
Mizengo Kayanza Peter Pinda lililoko Zuzu, nje ya Manispaa ya Dodoma,
kujionea wenyewe shughuli mbalimbali za kilimo cha mazao mbalimbali na
ufugaji wa mbuzi na nyuki. Humo kunalimwa nyanya, vitunguu, mboga mboga,
migomba, mapapai na matunda mengine mengi, bila kusahau zao ambalo ni
alama ya Dodoma, Zabibu. Hapa wako katika picha wakiwa wamepumzika baada
ya kuzunguka kwenye shamba hilo kubwa. Wanasema 'ukienda hutamani
kutoka' kutokana na mazao yaliyomo humo. Pengine walinyimwa' mahindi ya
'gobo' ambayo yamo humo, vinginevyo 'kila mtu angekuwa anatafuna' hapa.
Mwimbaji wa
Kwaya ya Uinjilisti ya KKKT Usharika wa Kihesa ya mjini Iringa
akifurahia mandhari nzuri kwenye shamba la Waziri Mkuu Mhe. Mizengo
Pinda huko Zuzu, nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma. Wanakwaya hao wako
huko kwa ajili ya kuhubiri Injili na kesho wanatarajiwa kutembelea
Bungeni. ( Picha zote na msomaji wa www.brotherdanny5.blogspot.com)
Eti nyanya
zinapatikana Ilula peke yake,nani kakudanganya?! Mmoja wa waimbaji wa
Kwaya ya Uinjilisti ya Kanisa la KKKT Usharika wa Kihesa mjini Iringa
akifurahia kuona matunda ya mbegu bora za nyanya kwenye shamba la Waziri
Mkuu Mhe. Mizengo Pinda lililoko Zuzu, nje kidogo ya Manispaa ya
Dodoma.
Mbuzi zaidi
ya 100 wanafugwa kwenye shamba hili la Waziri Mkuu Mizengo Pinda,
ambalo liko Zuzu, nje ya Manispaa ya Dodoma. Ukiwa hapa utajifunza mambo
mengi ya kilimo na ufugaji, kwani kilimo cha mazao mengi kimesheheni
humo na kinaendeshwa na wataalamu kwa umwagiliaji.
Siyo lazima
usubiri ushauri wa daktari kwamba ule mapapai ndipo uanze kutafuta wapi
yanapatikana. Katika shamba la Waziri Mkuu Mizengo Pinda lililoko Zuzu,
nje ya Manispaa ya Dodoma, ameyapanda mengi na yanamwagiliwa kama hivi.Mahindi yamekauka kitambo Dodoma na watu wanavuna, lakini ndani ya shamba la Waziri Mkuu huko Zuzu, nje ya Manispaa ya Dodoma, hali ni tofauti kabisa. Bado 'gobo' inapatikana. Ni kutokana na kilimo cha umwagiliaji.
Hata vitunguu vinastawi, tena kwa umwagiliaji. Ni ndani ya shamba la Waziri Mkuu huko Zuzu.
Unadhani migomba inastawi Moshi, Mbeya na Kagera tu? Njoo Zuzu kwenye shamba la Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda uone. Mzuzu, Mshale, Bukoba na kadhalika zote zinapatikana hapa.
Shamba hili lilikuwa na kokoto nyingi sana, kwa mujibu wa maofisa wanaolisimamia. Ingekuwa kama kule Iringa, 'wapwa' zangu Wanyalu wangeseme; "Bhe, unanipa shamba lenye kokoto litalifanyaje!" Lakini kokoto hizi zmechimbuliwa, shamba likasawazishwa tayari kwa kilimo. Matokeo yake ni kwamba, kokoto nazo ni dili la nguvu, kama hujengei wewe, unaweza kuziuza ukapata 'mpunga' wako, safi kabisa. Hili ni somo kubwa sana kwa Watanzania, hata wa hali ya kawaida, katika kupanga matumizi ya ardhi yao.
Inahitaji mtaji wa kutosha kuhudumia shamba kama hili le Mhe. Waziri Mkuu Pinda. Nyenzo kama matrekta ni muhimu, lakini hata kama huna lako, waweza kukodisha.
Halafu pia anafuga kweli nyuki. Ona mizinga ilivyopangana. Fursa zipo jamani, tuzikamate na kuzitumia na itawezekana ikiwa serikali nayo itawawezesha wakulima hata mitaji kupitia vikundi vyao.
Embe
zimesheheni ndani ya shamba hili la Mhe. Pinda lilipo Zuzu, nje kidogo
ya mji wa Dodoma. Kumbe kila sehemu tunaweza kupanda mazao mbalimbali
ikiwa tutazingatia ushauri wa wataalamu pamoja na kuwepo kwa miundombinu
bora, hasa upatikanaji wa maji.
Jamani
Dodoma aaaa, Dodoma ya Watanzania aaaa! Naam, na Zabibu ndilo zao kuu la
biashara mkoani Dodoma ukiacha karanga na alizeti na Mhe. Mizengo Pinda
naye alimelipa kipaumbele kwa kulima kitaalamu kabisa akitumia
umwagiliaji wa matone kama kule Israel. Zao hili linastahimili sana
ukame na kwa sasa lina soko kubwa mjini Dodoma ambako inaelezwa viko
viwanda takriban vitatu vikubwa kabisa vinavyotengeneza mvinyo. Kwa kuwa
malighafi ni zabibu, wananchi wanahimizwa kulima kwa wingi ili kukidhi
mahitaji ya viwanda hivyo.
Habari kwa hisani ya http://brotherdanny5.blogspot.com
No comments
Post a Comment