Writen by
sadataley
1:33 PM
-
0
Comments
Mwadhama Polykarp Kardinali Pengo ©Dar es Salaam Arch Diocese |
"Hakuna taifa lililoendelea bila watu wake kupata elimu" Ni maneno ya
Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati wa hafla ya kuweka jiwe la
msingi la ujenzi wa chuo kikuu cha Marian, kilichopo chini ya Chuo Kikuu
cha Mtakatifu Agustino.
Padri Valentino Bayo anasema kuwa wamefikia hatua hiyo kama hatua ya
kuiunga mkono serikali katika kukuza masomo ya sayansi, maana taifa
limepungukiwa kwenye sekta hiyo. Bayo ambaye ni meneja wa shule za
Marian ambayo iko kuanzia shule ya msingi hadi sasa kuelekea elimu ya
juu, amewataka watu kujikita kwenye elimu kwa kadri wawezavyo.
Mfuko wa hifadhi ya jamii wa ppf umehusika kwenye tukio hilo ambapo
michango mingine imepatikana kwa njia ya wanafunzi na harambee
iliyofanyika kwenye hafla hiyo jijini Bagamoyo, mkoani Pwani.
Habari na Gospel Kitaa
No comments
Post a Comment