Writen by
sadataley
4:13 PM
-
0
Comments
Polisi wa Ukraine wanasema kuwa
zaidi watu 30 wameuawa katika moto ulioanza baada ya makabiliano kati ya
vikosi vya wanamgambo wanaounga mkono Urusi na wafuasi wa serikali
katika mji wa kusini magharibi wa Odessa.
Haijulikani ni nini kilichosababisha moto huo
katika jengo la chama cha wafanyikazi ,huku ripoti zikiarifu kwamba
pande zote mbili zilikuwa zikitumia mabomu ya petroli."Waziri wa mpito wa Mambo ya Ndani nchini Ukraine Arsen Avakov amesema kuwa harakati za serikali kudhibiti mji wa mashariki wa Sloviansk uliopo mashriki mwa Ukraine zinaendelea na kwamba vikosi vyake vimeliteka jengo la Televisheni karibu na Kromartosk."
Naibu waziri wa maswala ya kigeni nchini Ukraine amesema kuwa bila kujali ni nani aliyeuawa, mauaji hayo ni janga kubwa.
Ameitaka mamlaka ya Urusi kusitisha vitendo vya maafisa maalum ambao huenda wakadhoofisha usalama wa eneo hilo.
Hata hivyo habari hizo hazijathibitishwa.
Wakazi wamethibitisha kuwa kumekuwa na vita vikali katika eneo hilo huku wengine wakijaribu kulizuia jeshi la Ukraine kuingia katika eneo hilo.
Wizara ya Ulinzi mjini Kiev imesema kuwa magharibi mwa Sloviansk kumekuwa na mapigano makali ambapo vikosi vya Ukraine vilivamiwa na makundi yaliojihami na kusababisha mauaji ya wanajeshi wawili wa Ukraine.
No comments
Post a Comment