Writen by
sadataley
1:23 PM
-
0
Comments
Na Waandishi Wetu, Mwananchi
Dodoma. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uratibu
na Uhusiano), Stephen Wassira amewatisha wabunge wa Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa), kwamba wasiporejea bungeni, kanuni zitabadilishwa na
Bunge litaendelea.
Wassira alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati
akijibu hoja za wabunge mbalimbali akiwamo Mbunge wa Kawe (Chadema),
Halima Mdee kuwa majadiliano ndani ya Bunge la Katiba yanakiuka Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba.
Katika mchango wake, Mdee alisema Ukawa hawako
tayari kurejea ndani ya Bunge Maalumu la Katiba Agosti, mwaka huu endapo
majadiliano ya Katiba hiyo hayatajikita kwenye Rasimu ya Pili ya
Katiba.
Hata hivyo, Wassira akijibu kauli hiyo ya Mdee na
wabunge wengine waliopaza sauti kuhusu kukiukwa kwa sheria hiyo alisema:
“Kama hamrudi tutatumia kanuni zile kutafuta akidi na Bunge
litaendelea.”
“Tusigeuze Bunge hili kuwa Bunge la Katiba… Bunge
la Katiba lipo tena lipo kisheria…. Kuna watu wanageukageuka wanasema
sheria ilivunjwa, lakini hawasemi kifungu gani kilivunjwa,” alisema
Wassira.
Wassira alisema wajumbe wa Bunge la Katiba
walitunga Kanuni za Bunge hilo na miongoni mwa waliokuwa walimu wa
kanuni hizo alikuwa Ismail Jussa na Tundu Lissu ambao ni wajumbe wa
Ukawa.
“Kanuni tuliyotunga ambayo haipingani na Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba ni Bunge hilo kuwa na mamlaka ya kubadili,
kurekebisha, kuboresha na kadhalika,” alisema Wassira na kuongeza:
“Sasa leo wenzetu baada ya kuamua kutoka wanasema
tunavunja sheria eti kwa sababu tunapingana na mawazo ya wananchi. Hiyo
siyo sawa. Tunapingana na maoni yapi ya wananchi?
Wassira alisema kama ni hoja ya maoni ya wananchi,
upande wa Zanzibar asilimia 60 walitaka Serikali ya mkataba lakini
rasimu iliyopo mbele ya Bunge Maalumu la Katiba haina mapendekezo ya
mkataba.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick
Werema aliwasihi wajumbe wa Ukawa warejee bungeni, akisisitiza kuwa
Katiba Mpya itapatikana kwa maridhiano na si kwa wajumbe kuasi Bunge.
Mabilioni Bunge la Katiba utata
Wabunge wa upinzani wamehoji kiasi cha fedha
kilichotumika kugharimia awamu ya kwanza ya Bunge Maalumu la Katiba.
Kuhoji huko kumetokea wakati, Wizara ya Katiba na Sheria ikisema Sh21
bilioni zimetengwa kwa ajili ya awamu ya pili ya Bunge la Katiba
linalotarajia kuanza vikao vyake Agosti 5, mwaka huu mjini Dodoma.
Kwahabari zaidi ingia http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Wassira-awatisha-Ukawa/-/1597296/2316498/-/mgd180z/-/index.html
Kwahabari zaidi ingia http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Wassira-awatisha-Ukawa/-/1597296/2316498/-/mgd180z/-/index.html
No comments
Post a Comment