Writen by
sadataley
1:34 PM
-
0
Comments
Na Beatrice Moses, Mwananchi
Dar es Salaam. Wakati Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa), ukitarajiwa kuanza ziara ya siku 10 katika mikoa ya
Tanzania Bara kesho, viongozi wa umoja huo wamemvaa Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana kwa kauli yake kuwa Katiba haina umuhimu.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema
jana kwamba ameshangazwa na kauli ya Kinana kwa kuifananisha Tanzania na
Uingereza ambayo haina Katiba.
“Kauli hii imenipa matatizo, naanza kutilia shaka
kisomo cha hawa wenzetu...“Hawana Katiba ya kuandika lakini wana sheria
zao ambazo wanaziheshimu, ndiyo maana huwezi kuwahoji kuhusu Malkia
Elizabeth wakakuelewa.
Mikutano ya Ukawa
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF),
Julius Mtatiro alisema awamu ya kwanza ya ziara hiyo itaanza kesho hadi
Mei 26, mwaka huu.
Alisema ili kufanikisha ziara hiyo, Ukawa imejigawa katika timu tatu ambazo zitakuwa zinafanya mikutano na maandamano ya amani.
Kundi la kwanza litaongozwa na Katibu Mkuu wa
NCCR- Mageuzi, Mosena Nyambabe, la pili litakuwa na Dk Slaa na la tatu
litakuwa chini ya Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba.
No comments
Post a Comment