Writen by
sadataley
1:35 PM
-
0
Comments
Na Joseph Zablon, Mwananchi
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal wamejumuika na mabalozi mbalimbali nchini wamejumuika kuuaga mwili wa aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Flossy Gomile-Chiyaonga.
Mbali ya Viongozi hao pia watu mbalimbali
walijitokeza kuuaga mwili wa Balozi huyo jana kwenye ukumbi wa Mwalimu
Julius Nyerere walipotoa heshima zao za mwisho.
Mwili wa balozi huyo unatarajiwa kuzikwa mjini
Blantyre nchini Malawi kesho na marehemu alifariki dunia Ijumaa
iliyopita baada ya kupoteza fahamu ghafla akiwa nyumbani kwake na
alipokimbizwa hospitalini ilibainika kuwa aliishapoteza maisha.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe ambaye ataiwakilisha Tanzania
katika msiba huo, alisema kuwa serikali itatoa ndege itakayosafirishwa
mwili huo hadi mjini Blantyre.
Alisema balozi huyo ambaye aliripoti nchini miaka
miwili iliyopita, alikuwa kiungo muhimu baina ya Tanzania na Malawi na
alikuwa mtu ambaye anapenda kujielimisha na kujumuika na wengine wakati
mwingi bila kujali hadhi yake.
Alibainisha kuwa balozi Gomile Chidyaonga alitumia
muda wake mwingi kutafuta elimu na kutokana na hali hiyo mara kwa mara
amekua akishiriki midahalo ya kitaaluma iliyokuwa inafanyika Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (UDSM) na alikuwa kiungo muhimu wakati wa mgogoro wa
mpaka baina ya nchi mbili.
“Tumepoteza kiungo muhimu baina ya mataifa haya
mawili na amefariki wakati akiwa katika harakati za kuelekea nchini humo
kwa likizo ya kawaida na ilikuwa aondoke Alhamisi lakini kwa kuwa
alikuwa hajisikii vizuri alisema ataifanya safari yake Ijumaa,” alisema
Membe.
Awali akizungumza katika hafla hiyo, Balozi mdogo
wa Malawi nchini, Kwacha Chisiza alisema kuwa nchi hiyo imepata pengo
kubwa kutokana na kumpoteza balozi huyo msomi ambaye pia aliwahi kuwa
mkuu wa vitivo viwili tofauti katika Chuo Kikuu cha Malawi.
Chisiza alisema kuwa balozi huyo pia aliwahi
kushika wadhifa kama huo katika nchi za Rwanda, Shelisheli, Uganda,
Burundi na balozi mdogo nchini Uingereza na taarifa za kitabibu
zilieleza kuwa balozi huyo alifariki kutokana na kupasuka mshipa mkubwa
wa moyo hivyo kutiririsha damu mwilini na kusababisha kifo chake
No comments
Post a Comment