Writen by
sadataley
3:28 PM
-
0
Comments
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa wa Chadema, John Heche
Na Waandishi Wetu, MwananchiDodoma. Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) nje ya Bunge umesema
hatima ya kupata Katiba Mpya utaamuliwa na wananchi na wala siyo chama
tawala.
Kauli hiyo inatolewa ikiwa ni siku moja baada ya
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uratibu na Uhusiano), Stephen Wassira
kusema Ukawa wasiporejea bungeni, kanuni zitabadilishwa na Bunge
litaendelea.
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa wa Chadema, John Heche alisema hakuna nchi inayoandika Katiba kwa kushirikisha kundi moja.
Alisema Ukawa hawatarejea bungeni pamoja na
vitisho vinavyotolewa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya CCM hadi
pale mjadala wa kuijadili Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba
utakapozingatiwa.
“Acha wajidanganye kubadili kanuni, lakini mwisho
wa siku wananchi wanajua kinachofanywa na CCM, hatima ya Katiba Mpya iko
mikononi mwao,’ alisema Heche na kuongeza:
“CCM haina nia ya kupata Katiba Mpya, kwani
viongozi wake wamekuwa wakisema Katiba iliyopo inafaa, jambo ambalo
tunashindwa kuelewa kwa nini imetoa mabilioni kuratibu mchakato huu.”
Katika hatua nyingine, Jumuiya na Taasisi za
Kiislamu Tanzania imejiunga na Ukawa unaoundwa na vyama vya Chadema,
NCCR-Mageuzi na CUF katika mikutano inayoendelea nchi nzima.
Msemaji wa Jumuiya hiyo, Sheikh Rajabu Katimbo alisema malengo mazuri ya Ukawa ndiyo yaliyowashawishi kujiunga.
Alisema taasisi zake zimeunga mkono harakati za
Ukawa kutokana kwa vile CCM imedhamiria kutupa kutupa maoni ya wananchi
kupitia Rasimu ya pili ya Katiba iliyowasilishwa bungeni na Mwenyekiti
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
juzi katika Viwanja vya Mwembetogwa mjini hapa, Katimbo alisema
kilichofanywa na Wajumbe wa Bunge la Katiba kutoka CCM ni ukiukwaji wa
haki kwa wananchi.
No comments
Post a Comment